Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 7, 2022

MAONYESHO YA KUSOMA QURAN WATOTO WANGUA VILIO BAADA YA KUGUSWA NA UJUMBE.





  Mtoto Hasra  Abdulrahaman  akifutwa Machozi na Mama yake wakatia akisoma Quran


                     Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

BAADHI ya watoto wa Madrassa  ya Al- Hasaniyyah walioshiriki Maonyesho ya Watoto ya Kusoma Quran wamemwaga machozi  wakati wakisoma Quran. 

 

Onyesho hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Morogoro’OCD’ SP Georgna  Matagi limefanyika Juzi Jumamosi  Makao Makuu ya Madrassa hiyo Msikiti wa Kingo uliopo Masika Mkoani hapa.

 

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi aliyealikwa kwenye hafra hiyo iliyofana vilivyo  mmoja wa watoto  walioangua Vilio Hasra  Abdulrahaman alisema.

 

Ujumbe mzito wa aya aliyosoma ulimgusa moyoni na kujikuta akishindwa kujizuia na kujikuta akimwaga machozi.

 

Kufuatia hali hiyo Mgeni rasm OCD ambaye kiimani ni Mkristo naye aliguswa na jambo hilo na kuamua kuwatunza pesa watoto hao.

Picha za tukio hilo la OCD SP Georgna  kuwatunza pesa watoto hao zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...