...Afande Sanya akimlima kadi mchezaji wa Yanga Jaja
Martin Sanyaa akikabidwa zawadi baada ya kuibuka kuwa refa bora wa ligi kuu Taznaia Bara misimu kadhaa iliyopita
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
TOKA ligi kuu Tanzania bara ilipoanza Agost Mwana Jana Mwamuzi Maarufu Tazania Afande Martin Sanyaa hakuonekna na Geji ya FIFA aliyokuwa nayo zaidi ya miaka 5.
Hali hiyo imezua mjadara mzito kutoka kwa Mashabiki wa Soka nchini kila mmoja akisema lake juu ya tukio hilo.
Mijadara hiyo imeshuhudiwa na Mwandishi wa Mtandao huu mara kadhaa kwenye Mabanda ya Video’ Maarufu ‘Vibanda Umiza’ wakati mashabiki hao wakimshuhudia kwenye Luninga refa huyo ambaye ni Askari Magereza wa gereza la Manispaa Morogoro akichezesha mechi kubwa za ligi kuu huku akiwa hana beji hiyo ya FIFA kifuani.
Baadhi ya mshabiki hao walisema refa huyo amepokonywa beji hiyo ya FIFA baada ya uwezo wake wa uchezeshaji kushuka.
Wengine walipinga kwa hoja kwamba refa huyo aliyewahi kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga zaidi ya mara 3 bado anauwezo mkubwa wa kuzitafsi sheria 17 za mchezo wa Soka Duniani.
Kufuatia mabishano hayo Mwandishi wa Mtandao huu juzi aliamua kumtafuta refa huyo kwa lengo la kupata ufafanuzi kuhusiana na tukio hilo.
“ Shekidele naona ulinipigia nilikuwa kwenye kikao nimekuta Miss Call yako”alisema Afande huyo na alipotakiwa kuelezea jambo hilo alijibu.
”Nikwe msimu huu sikupewa beji ya FIFA hii ni kwa sababu ya maradhi,gemu yangu ya mwisho kuchezesha msimu uliopita ni fainali ya michuano ya Simba Cup kati ya wenyeji Simba na TP Mazembe ya Kongo.
Baada ya kukamilika kwa gemu ile nilipara maradhi ya nyonga iliyopilekea nikae nje ya uwanja nusu msimu sikuchezesha mchezo yoyote hivyo nikakosa sifa za kupata beji hiyo ya FIFA.
Namshukuru Mungu kwa sasa nimepona kabisa kama ulivyonishuhudia naendelea kuchezaji bechi za ligi kuu huenda msimu ujao nikarejeshewa beji hiyo ya FIFA.”alisema refa huyo aliyewahi kuwa refa bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara na kukabidhiwa zawadi na waliokuwa wadhamini w aligi hiyo kampuni ya zimu za Mkononi ya Vodacom
No comments:
Post a Comment