Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, March 23, 2022

BINGWA WA DISCO ATUNZWA PESA NA MWANAYE AKIUWASHA MOTO UKUMBINI.

"Baba yangu mzazi bado wao' ni kama anasema Chichi Maneno Ngedere akimtunza Mpesa baba yake mzazi Maneno Ngedere aliyeuwassha Moto kwenye Send Off  Sweet Athuman Ngedere Mtoto wa mdogo wake

BABA NA MWANA, Maneno Ngedere akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu juzi akiwa na bint yake wa kwanza
Bingwa wa kusakata disko Afrika Mashariki na Kati Maneno Super Ngedere akiuwasha Moto juzi kwenye send Off ya bint yake
Maneno Ngedere'Kulia' akimpongeza Mdigi wake Athuman Ngedere kwa kukuza na kufikia hatua ya kuozesha

 

...Athumani Ngedere akiwa na Mwanaye Chichi Maneni Ngedere ambaye ni Mtoto wa kwanza wa Kaka yake, Picha Juu Maneno Ngedere akipozi kwenye kamera za Mtandao huu akiwa na bint yake.


Send  Off hiyo ya  Familia ya Ngedere ilifanyika kwenye Ukumbi huu wa Kisasa unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

 Chini ni Madunia na eneo lote la Juu ni ukumbi mKubwa wa kufanyia shughuyri mbali mbali.kama vile Mikutano Send Off na harusi.

 Bei  ni nafuuu sana hivyo wasiliana na Afsia biashara wa Manipaa kama unahitaji ukumbi huo uliopo katikati ya Mji wa Morogoro.

 


                    Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Bigwa wa kusakata disco Afrika Mashariki na Kati Maneno Ngedere'Super Ngedere' ameuwasha Moto ukumbini na kutunzwa Pesa na bint yake wa kwanza Chichi Maneno Ngedere' .

 

Tukio hilo lilitokea juzi Jumapili kwenye Sherehe ya Kumuaga  Sweet Athuman Ngedere iliyofanyika  Ukumbi wa Mbaraka Mwishehe uliopo  Nunge Manispaa ya Morogoro.

 

Chichi aliyefunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja kwenye Send Off ya Mdogo wake alivutiwa na uchezaji wa baba yake Mzazi na kuamua  kumtunza Pesa.

 

lfahamike Chichi ameolewa Jijini Dar na amejaliwa kupata Mtoto mmoja, na kwenye Send Off hiyo alijumuika na wanadugu wengine kubadili mavazi kila tukio la shughuri hiyo.

 

Nilivyopost jana habari na matukio ya Send Off  hiyo ya Familia  ya Ngedere watu wengi walikuja ln boks na wengine kunipigia simu wakitaka kuona Picha ya Staa Asha Ngedere.

Nilipongia kwenye Send hiyo majira ya saa 3 usiku nikitokea kwenye Mashindano ya Magari cha kwanza nilianza kumtafuta Asha Ngedere ukumbini sikubahatika kumuona.

 

Nikaamua kumuliza baba wa shughuri hiyo Athuman Ngedere akanipa majibu haya.

“Shekidele Sister Asha amesafiri yuko Dar lakini siku ya Ndoa atakuwepo”alisema.

 

Baada ya kuona wadau wengi wa Mtandao huu wanazidikupiga simu wakiwa na shahuku kumbwa ya  kuona Picha ya Asha Ngedere kwa vile wengi wao hawamfamu kwa sura jana niliamua kumtwangia simu.

“ Niko Dar naludi Alhamis nikifika Moro nitakupigia unipige hiyo Picha wanayoulizia wadau wako”alisema Asha Ngedere. 2 Picha no1 Maneno'Super Ngedere'

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...