Maderena kutoka Moshi wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo jana.
...Wakitimua vumbi kusaka ushindi baada ya kuruhusiwa
Utamu wa mshindano ya magari ni kwenye kona mashabiki hawa wamejazana kwenye Mnada ya Ng'ombe, Mbuzi na Kondoa wa Tubuyu Nane nane kwenye kona 3 za mashindano hayo huku wengine wakiamu kupanda juu wa mti kufaidi zaidi uhondo huo, ahapo hapo madereva walionyesha michezo mikali kwenye kona hizo, ambapo baadhi magari yao walipata kichomi kwenye kona hizo na kutoka mshindanoni
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ni Mwandishi Pekee kutoka Moro aliyepewa Mwaliko kwenye mashindano hayo akitoka kwenye hotel ya Morena huku akiwa na kibari Maarumu shingoni cha kupiga Picha maeneo yote ya mshindano hayo
‘Press Card’.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Dereva G.S Dhambi na Msoma ramani wake R. lsmail wameibuka washindi kwenye mbio za kimataifa za Magari zilizofanyika jana jumapili kwenye Mashamba ya Mkonge yaliyopo Kando kando ya barabara kuu ya Moro-Dar Mtaa wa Tubuyu Nane Nane Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro.
Toka Mashindano hayo yalipo anza majira ya saa 2 asubuhi Mwandishi wa Mtandao huu aliwatabiria ushindi ‘Mabwashee’ hao kutoka Moshi Mkoa wa Kilimanjaro Tanzania na dereva kutoka Kampala Uganda kwamba huenda wakaibuka washindi kutokana na Ubora wa magari yao ambapo kwenye ukaguzi wa njia uliofanyika juzi walionekana kuwa bora zaidi ya wenzao.
Mashindano hayo yalishirikisha madereva 17 kutoka Uganda, Kenya na Wenyeji Tanzania huku magari zaidi ya saba yakishindwa kuendelea na mashindano baada ya kuharibika akiwemo mkenya mmoja.
Picha za gari lake Mkenya huyo likivutwa zitaruka hewani hivi punde sambamba na matukio mengine ya mashindano hayo.
Hafra ya makabidhiano ya zawadi kwa washindi yalifanyika jana jioni katika hotel ya kisasa ya Morena iliyopo Msamvu jirani na Stend ya Mabasi ya Mikoani,
lfahamike hotel hiyo ya ‘Planet Kadhaa’inamilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Gairo Mh Ahmed Shabiby ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Mabasi bora na ya Kisasa ya Shabiby Line.
No comments:
Post a Comment