Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, March 22, 2022

KHADIJA YUSUFU ANONGESHA SEND OFF YA FAMILIA YA NGEDERE.

Khadija Yusuf kulia akiimba kwenye Send Off hiyo juzi huku  Perereza Ganzer kushoto ambaye ni mama mzazi wa bi harusi Mteule akimtunza mwimbai huyo wa muziki wa taarabu nchini
                                            Khadija Yusuf
      Khadi Yusufu akiwa na Perereza Juma Ganzer kushoto
Bi harusi Mteule Wseet Athuman Ngedere akiingia ukumbini huku akisindikizwa na mabest wake



                             Sweeti katika Ubora wake



Bi harusi mteule kulia akiwa na baba yake mzazi Athuman Ngedere

Athuman Ngedere akiwa mkwe wake  ssa Salum Ally Mkazi wa  Buza Dar.Picha ya juu Athuman akiwa na bint yake Sweet


                   Athumna kulia akiwa na mkwe wake


                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MWIMBAJI Maarufu nchini wa muziki wa Mwambao Malkia Khadija Yusuf anayepiha kazi Jahazi Morden Taarab kwa sasa Safina juzi amenongesha Send Off ya Bi. Sweet Athuman Ngedele. Khadija ambaye anazaliwa’damu moja’  na Gwiji la taaraja nchini Mfalme Mzee Yusuf aliimba nyimbo tatu mfululizo huku akiwa ametinga Sale na wazazi wa Bi-harusi Mteule

 

Send Off hiyo ya kukata na shoka iliyojaa Mastaa wa Mujini imefanyika juzi Jumapili ndani ya Ukumbi wa Mubaraka Mwishehe unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

lkumbukwe ukumbi huo Mpya na wakisasa Upo maeneo ya Nunge zamani  ulijulikana kwa jina la DDC kabla ya kuvunjwa na kujengwa ghorofa baada ya kukamilika umezindulikwa Mwishoni mwa mwaka jana na kiongozi wa taifa wa Mbio za Mwenge.

Pesa inaongea kivutia kikubwa kwenye sherehe hiyo  ilikuwa shoo ya mavazi ambapo kila tukio Bi,harusi Mteule na wapambe wake walibadili nguo tena nguo za bei mbaya sio marapurapu ya mtumbani.

Sweet bint Ngedere  anatarajia kufunga ndoa wiki hii na Bw lssa Salum Mkazi wa Buza jijini Dar es salaam.

 

 lfahamike bibi harusi huyo Mteule anatoka  familia ya Mastaa baba yake Mkubwa Maneno Ngedere Maarufu Super Ngedere mpaka sasa anashikiria Ubingwa wa kusakata Disko Afrika Mashariki na Kati alioutwa miaka ya 90 akiwagaragaza Kanda Kids wa Kenya, Bob Tiger wa Morogoro,Marehemu Black Moses na Athumad Digadiga wa Dar.

 

Ant yake Asha Ngedere wakati kundi la Original Kodemedy wakati huo ilikiwa la Moto Chanel 5 mara kwa mara walikuwa wakimtaja kwenye Vichekezo vyao hali iliyomjengea umaarufu Mkubwa hapa nchini.

Huku baba zake wakubwa, Abdallah Ngedere, Ramadhan Ngedere na Mashaka Ngedele kwa miaka mingi wanaishi nje ya nchi.

Mashaka yuko Brazir Abdallah na Ramadhan wanaishi ltalia ingawa kwa sasa Ramadhan amerejea nyumbani  Morogoro.

 

Mwandishi wa Mtandao huu anaifahamu vizuri familia hiyo ya Marehemu Mohamed Ngedere na Mkewe Kidawa ambaye naye ametangulia mbele za haki,  kwa miaka Mingi Familia ya Mzee Ngedere na ile ya Mzee Shekidele waliishi nyumba Moja Kota za Paju zilizopo Mji Mpya.

 

Mtandao huu umekusanya Matukio kadhaa kwenye Send Off hiyo ikiwemo Densa Super Ngedere kuwasha Moto kwenye Send Off hiyo ya bint yake hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...