Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, March 1, 2022

KUMBUKIZI. HABARI YA KIJAMII ZAIDI.

Shekidele akizungumza na wazazi wa Mgonjwa huyo Kijijini kwao Kilosa,.sambamba na Mwandishi huyo kuwapa posho kidogo ya kujikimu, Familia hiyo nayo ilisambaza Upendo kw akumpoatia Mwandishi huyo zawadi ya Mkungu wa Ndizi
 

Na Mwandishi wetu
Mwandishi wa habari hizi anayejikita zaidi katika habari za Kijamii Mwaka 2012 alipokea taarifa kutoka Wilaya Kilosa kwamba kuna familia ‘Duni’ inauguza mtoto wao kwa muda mrefu aliyekumbwa na maradhi ya ajabu. 
 
Wakati Mwandishi huyo anapokea taarifa hiyo kwa njia ya simu alikuwa njia na Waandishi wenzie wakielekea kwenye semina yenye Posho a,k,a’Mshiko’. 
 
Kutokana na uzito wa habari hiyo ya kijamii. Mwandishi wa habari hizi aliamua kusitisha safari ya kuelekea kwenye semina hiyo.
Akiwaaga waandishi wenzie akiwaeleza kwamba amepata safari ya ghafra anaelekea Kilosa kufuatilia habari ya kijamii. 
 
Waandishi hao walishangazwa na Uamuzi huo huku baadhi yao wakisema “Shekidele kweli umeshiba pesa unaacha kazi ya mshiko unakwenda Kilosa kwenye kazi ya kujitolea. 
 
Shekidele aliwajibu kwa kinywa kipana”Hasara roho Pesa Makaratasi mimi ninawito moyoni wa kufanya kazi za wenye uhitaji na si kazi za kunufaisha Maisha yangu binafsi ili hali wengine wanauhitaji wa huduma yangu.” 
 
Baada ya kuwajibu Shekidele aliingia kituo cha Mafuta akajaza lita 6 za Petrol zilizotosha kutoka Moro Mpaka Kilosa kwenda na kuludi wakati huo lita Moja iliuzwa elfu 2. 
 
Jana niliripoti habari la Mwanume kufiwa na Mkewe kijijini kwake Dakawa Wilaya ya Movomero, Leo nimeripoti habari hii na kesho panapo majari ya mwenyezi Mungu nitaripoti habari nyingine ya Kijamii zaidi
                      

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...