Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, March 2, 2022

KUMBUKIZI. HABARI YA KIJAMII ZAIDI HII NI MWAKA 2013


 


 

 Na  Dunstan Shekidele,Morogoro.

Mfanyabiashara ndogo ndogo’Mmachinga’ Bw Jeremia Msafiri amekatwa mguu na Mkono na Treni wakati akifanya biashara Stesheni ya Kilosa.

Baada ya kutokea kwa ajari hiyo Kama kawaida Mwandishi wa habari hizi alipigia gia Pikipiki yake Mpaka nyumbani kwa Jeremia na kufanikiwa kuzungumza naye A-Z.

” Pole kwa safari hakika wewe ni Mwandishi wa Mfano hapa Kilosa kuna Waandishi wengi wa habari lakini habari hii haijaripotiwa popote toke nipate ajari takribani miaka 3 iliyopita.

Wewe umefunga safari kutoka Morogoro kwa gharama zako Mpaka hapa Kijijini, ubarikiwema sana”akisema Jeremia na kuendelea kudadavua ajari ilivyotokea.  

 

“Kama unavyojua Steshen Wilaya ya kilosa  ni ndogo Tren haikaa muda mrefu kuna abiria alinunua Machungwa matatu wakati akihangaika kutoa pesa kwenye Pochi Tren ameanza kuondoka nikatua Kapu la Machunga  nikaanza kuifukuza Yule abiria alikuwua muungwa akatondasha elfu Moja yangu.

 

Nilipoinama kuiokoa nimeteleza mguu na Mkono vikaangukia kwenye Reli nikasagwa ”alisema Jeremia na kuangua Kilio. 

Toka apate ajari hiyo Mkewe hajawahi kupunguza upendo na badala yake kwa miaka takribani 4 alibeba jukumu la kutunza familia hiyo ya Mume na watoto watuta kwa kulima Vibarua Mashambani na Msimu wa kilimo ulivyoisha alizunguka kwenye majumba ya watu kuomba Vibarua vya kufua au kufanya usafi majumbani ili apate pesa la kutunza familia yake.

Nyumba waliopanga awari kabla ya ajari  walihama baada ya kushindwa kulipa pango hivyo waliishi kwenye kinda kibovu kisicho na Mlango wa maana wala madirisha imara  huku juu  kikiezekwa kwa nyasi ambapo msimu wa Mvua kilivuja mara nyingine wakiwa usingizini.

Habari hiyo ya kusigitisha niliirusha hazeti la ljumaa huku nikiomba wadau kote nchini watakaoguswa na tukio hilo kumchangia chochote walichojaliwa. 

 

Nami niliwaachia nauli wakaja Mjini Morogoro nikazungumza na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bw Ngungamtiku kwa bahati alikubali Ombi langu akampokea Jeremia na Mkewe kwenye Kambi ya Kulea Wazee na Walemavu iliyopo eneo la‘Funga Funga’ Kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro.

 

Baada ya wiki Mbili  baadhi ya wasomaji wa gazeti la ljumaa kote nchini waliguswa na habari hiyo wakachangia kiasi cha Shiringi laki 6 kupitia simu yangu kufuatia Jeremia na Mkewe kukosa Simu na kuniamuru niweke namba zangu kwenye habari hiyo.

 Pichani nilimkabidhi Jeremia pesa hizo akiwa kambi ya Ustawi wa Jamii.

Kushoto Mkewe akivyoosha Mikono juu akimshukuru Mungu kwa Msaada huo. Baada ya kupata Pesa hizo waliamua kureja Kilosa kujiunga na watoto wao ambapo kwa maelezo yao Pesa hizo wamepanga kuziingiza kwenye Kilimo bora na nyingini kwenye Mtaji wa biashara. Mwandishi wa habari hizi anazidi kuwashukuru Watanzania wote waliomchangia ndugu yetu huyo Pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii kukubari kumpokea Mlemavu huyo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...