Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, March 27, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU LEO JUMAPILI


 

DANIEL 12

 

Mstari 8-10

 

Nami nikasikia lakini Sikuelewa, ndipo nikasema Ee Bwana Mungu,Mwisho wa Mambo haya Utakuwaje.?

 

Akasema enenda zako Daniel, maana maneno haya yamefungwa na kutiwa Muhuri,hata wakati wa Mwisho.

 

Wengi watajitakasa na kujifanya weupe na kusafika,  bali wabaya watatenda mabaya  wala  hataelewa Mtu Mbaya  awaye yote,bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.

 

Hili ndilo neno letu la leo Jumapili ya March 27.

Ambalo linatufundisha kwamba kwenye maisha yetu tusijikweze pia tusimuamini mtu kwa muonekano wa nje au kwa mavazi yake meupe au kwa Cheo chake ama utajiri wake.

Vile vile tusimuhukumu au kumdharau mtu kwa muonekano wake, kwa shida zake au kwa umasikini wake.

Thursday, March 24, 2022

MWAMUZI TANZANIA AFUNGUKA KUVULIWA BEJI YA FIFA.

              Mwamuzi Martin Sanya akiwajibika uwanjani
          ...Afande Sanya akimlima kadi mchezaji wa Yanga Jaja

 Martin Sanyaa akikabidwa zawadi baada ya kuibuka kuwa refa bora wa ligi kuu Taznaia Bara misimu kadhaa iliyopita


                          Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TOKA ligi kuu Tanzania bara ilipoanza Agost Mwana Jana Mwamuzi Maarufu Tazania Afande Martin Sanyaa hakuonekna na Geji ya FIFA aliyokuwa nayo zaidi ya miaka 5.

 

Hali hiyo imezua mjadara mzito kutoka kwa Mashabiki wa Soka nchini  kila mmoja akisema lake juu ya tukio hilo.

 

Mijadara hiyo imeshuhudiwa na Mwandishi wa Mtandao huu mara kadhaa kwenye Mabanda ya Video’ Maarufu ‘Vibanda Umiza’ wakati mashabiki hao wakimshuhudia kwenye Luninga refa huyo ambaye ni Askari Magereza wa gereza la Manispaa Morogoro akichezesha mechi kubwa za ligi kuu huku akiwa hana beji hiyo ya FIFA kifuani.

 

Baadhi ya mshabiki hao walisema refa huyo amepokonywa beji hiyo ya FIFA baada ya uwezo wake wa uchezeshaji kushuka.

 Wengine walipinga kwa hoja kwamba refa huyo aliyewahi kuchezesha mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga zaidi ya mara 3 bado anauwezo mkubwa wa kuzitafsi sheria 17 za mchezo wa Soka Duniani.

 

Kufuatia mabishano hayo Mwandishi wa Mtandao huu juzi aliamua kumtafuta refa huyo kwa lengo la kupata ufafanuzi kuhusiana na tukio hilo.

 

“ Shekidele naona ulinipigia nilikuwa kwenye kikao nimekuta Miss Call yako”alisema Afande huyo na alipotakiwa kuelezea jambo hilo alijibu.

 

”Nikwe msimu huu sikupewa beji ya FIFA hii ni kwa sababu ya maradhi,gemu yangu ya mwisho kuchezesha msimu uliopita ni  fainali ya michuano ya Simba Cup kati ya wenyeji Simba na TP Mazembe ya Kongo.

 

Baada ya kukamilika kwa gemu ile nilipara maradhi ya nyonga iliyopilekea nikae nje ya uwanja nusu msimu sikuchezesha mchezo yoyote hivyo nikakosa sifa za kupata beji hiyo ya FIFA.

 

Namshukuru Mungu kwa sasa nimepona kabisa kama ulivyonishuhudia naendelea kuchezaji bechi za ligi kuu huenda msimu ujao nikarejeshewa beji hiyo ya FIFA.”alisema refa  huyo aliyewahi kuwa refa bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara na kukabidhiwa zawadi na waliokuwa wadhamini w aligi hiyo kampuni ya zimu za Mkononi ya Vodacom

Wednesday, March 23, 2022

BINGWA WA DISCO ATUNZWA PESA NA MWANAYE AKIUWASHA MOTO UKUMBINI.

"Baba yangu mzazi bado wao' ni kama anasema Chichi Maneno Ngedere akimtunza Mpesa baba yake mzazi Maneno Ngedere aliyeuwassha Moto kwenye Send Off  Sweet Athuman Ngedere Mtoto wa mdogo wake

BABA NA MWANA, Maneno Ngedere akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu juzi akiwa na bint yake wa kwanza
Bingwa wa kusakata disko Afrika Mashariki na Kati Maneno Super Ngedere akiuwasha Moto juzi kwenye send Off ya bint yake
Maneno Ngedere'Kulia' akimpongeza Mdigi wake Athuman Ngedere kwa kukuza na kufikia hatua ya kuozesha

 

...Athumani Ngedere akiwa na Mwanaye Chichi Maneni Ngedere ambaye ni Mtoto wa kwanza wa Kaka yake, Picha Juu Maneno Ngedere akipozi kwenye kamera za Mtandao huu akiwa na bint yake.


Send  Off hiyo ya  Familia ya Ngedere ilifanyika kwenye Ukumbi huu wa Kisasa unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

 Chini ni Madunia na eneo lote la Juu ni ukumbi mKubwa wa kufanyia shughuyri mbali mbali.kama vile Mikutano Send Off na harusi.

 Bei  ni nafuuu sana hivyo wasiliana na Afsia biashara wa Manipaa kama unahitaji ukumbi huo uliopo katikati ya Mji wa Morogoro.

 


                    Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Bigwa wa kusakata disco Afrika Mashariki na Kati Maneno Ngedere'Super Ngedere' ameuwasha Moto ukumbini na kutunzwa Pesa na bint yake wa kwanza Chichi Maneno Ngedere' .

 

Tukio hilo lilitokea juzi Jumapili kwenye Sherehe ya Kumuaga  Sweet Athuman Ngedere iliyofanyika  Ukumbi wa Mbaraka Mwishehe uliopo  Nunge Manispaa ya Morogoro.

 

Chichi aliyefunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kuja kwenye Send Off ya Mdogo wake alivutiwa na uchezaji wa baba yake Mzazi na kuamua  kumtunza Pesa.

 

lfahamike Chichi ameolewa Jijini Dar na amejaliwa kupata Mtoto mmoja, na kwenye Send Off hiyo alijumuika na wanadugu wengine kubadili mavazi kila tukio la shughuri hiyo.

 

Nilivyopost jana habari na matukio ya Send Off  hiyo ya Familia  ya Ngedere watu wengi walikuja ln boks na wengine kunipigia simu wakitaka kuona Picha ya Staa Asha Ngedere.

Nilipongia kwenye Send hiyo majira ya saa 3 usiku nikitokea kwenye Mashindano ya Magari cha kwanza nilianza kumtafuta Asha Ngedere ukumbini sikubahatika kumuona.

 

Nikaamua kumuliza baba wa shughuri hiyo Athuman Ngedere akanipa majibu haya.

“Shekidele Sister Asha amesafiri yuko Dar lakini siku ya Ndoa atakuwepo”alisema.

 

Baada ya kuona wadau wengi wa Mtandao huu wanazidikupiga simu wakiwa na shahuku kumbwa ya  kuona Picha ya Asha Ngedere kwa vile wengi wao hawamfamu kwa sura jana niliamua kumtwangia simu.

“ Niko Dar naludi Alhamis nikifika Moro nitakupigia unipige hiyo Picha wanayoulizia wadau wako”alisema Asha Ngedere. 2 Picha no1 Maneno'Super Ngedere'

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...