Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, February 4, 2022

ASKOFU AFUNGISHA NDOA 35 KWENYE IBADA MOJA

Maharusi wakiunganishwa kuwa mwili mmoja na Askofu Msimbe
Askofu Msimbe akiwaongoiza Mapadri kuingia kanisa Katoriki Parokia ya Dumila
....Maharusi 35 katika ubora wao wakijianda kufunga ndoa

Askofu wa kanisa Katoriki Jimbo la Morogoro Radharus Msimbe, akihubiri kwenye lbada hiyo

                Bibi harusi akisaini cheti chake cha ndoa
Wahooo Maharusi wamependeza wakionyesha shahada zao [Vyeti vya ndoa]

 ...Maharusi wakitoa shukrani zao kwa Askofu Msimbe mara baada ya kuunganishwa kuwa mwili Mmoja

.

                   Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

KATIKA hali ya kukabiliana na uchumba Sugu,Askofu Rodharus Msimbe wa  Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Jumapili iliyopita aliwaunganisha wanandoa 35 ambao kwa sasa wanaishi maisha ya kumpendeza Mungu.

 

Wanandoa hao waliamua kwa hiyari yao  kupasha Moto Kipora’Kufunga ndoa’ kwenye kanisa hilo Parokia ya Dumila  Wilaya ya Kilosa Mkoani hapa,kufuatia baadhi yao kuishi kwenye uchumba sugu kwa miaka Mingi.

 

Akihuribi baada ya kuwaunganisha wanandoa hao, Askofu Msimbe alikemea tabia za baadhi ya watu kuishi kwenye uchumba sugu kwa miaka Mingi jambo linalomchukiza Mwenyezi Mungu.

 

“Umeona tumechukua muda mfupi kufungisha ndoa hizi niwapongeza wanandoa wote kwa kutambua umuhimu wa kufunga ndoa, pia na upongeza Uongozi wa Parokia hii ya Dunila.

 

 Kwa mafundisho mazuri kwa waumini wetu yaliyopelekea yao kutambua uhuhimu wa kufunga ndoa na kuachana na maisha ya dhambia ya kuishi kinyumba” alisema Askofu huyo ambaye amesimikwa Uaskofu hivi karibuni akichukua nafasi ya Askofu Teresphori Mkude aliyestaafu kwa mujibu wa sheria za kanisa hilo kubwa duniani.

 

Mara baada ya ibada hiyo kukamilika baadhi ya maharusi hao Walirejea majumbani kwao kwa Miguu huku wakishikana Mikono,wengine walipakizana kwenye baiskeli zao, Boda boda na baadhi yao kwenye Magari.  

 

Mtandao huu unawapongeza Maharusi wote kwa hatua hiyo muhimu kwenye Maisha ya Mwanadamu, sambamba na kulipongeza kanisani Katoliki kwa kuratibu zoezi hilo.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...