Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, February 7, 2022

MKUFUNZI AWATAKA WAFANYAKAZI NCHINI KUISHUKURU SERIKALI.

Mkufunzia Mattaka akizungumza na Wakuu wa Vitengo vya PSSSF



 Wajumbe wakifuatilia kw amakini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye Semina hiyo


                                     Na Dunstana Shekidele,Morogoro. 

MKUFUNZI Maarufu Afrika Bw David Mattaka amewataka wafanyakazi  nchini kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuanzisha Mifuko ya hifadhi ya Jamii ukiwemo Mfuko wa PSSSF.

Bw Mattaka aliyasema hayo kwenye Semina ya siku 7 iliyoshirikisha Wakuu wa Vitendo vya P.S.S.S.F kutoka Mikoa Mbali Mbali ya Tanzania iliyofanyika Ukumbi wa Hedema Mkoani hapa.

 

”Wenzetu wazungu wanautamaduni wa kuhifadhi sehemu ya Pesa kwa lengo la kumsaidi mbele ya safari atakapoishiwa nguvu za kufanya kazi au biashara, sisi tumekuwa wagumu kidogo kufanya hivyo tukipata Mshahara tunautafuna wote tukiamini kwa Mwisho wa mwezi utapata tena.

 

Wengi wetu hatukuwa na malengo kwamba siku ukistaafu au kuacha kazi utapata wapi pesa za kuendesha maisha, hivyo kwa kutambua hilo Serikali ya Tanzania imeamua kuanzishi Mifuno hii ya Jamii ikimege sehemu ya Pesa zetu na kuzipeleka kwenye Mifuko hiyo na kutuhufadhia”alisema Mzee Mattaka ambaye  alikuwa mkufunzi wa semina hiyo.

 

Mara baaada ya kukamilika kwa semina hiyo iliyoanza Jumatatu iliyopita na kukamilika ljumaa Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ni Mwandishi Pekee aliyealikwa kwenye Semina hiyo alifanya mahojiano Maalumu na Viongozi wakuu wa Semina hiyo.

Clip Video za Mahojiano hayo zitaruka hewani hivi punde kwenye You Tube ya Shekidele.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...