Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, January 11, 2022

TANZIA. MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MORO AUNGANA NA RAIS SAMIA KUOMBOLEZA VIFO VYA WAANDISHI WA HABARI 6

                             Mh Rais Samia Suluhu Hassani
                                Husna Mlanzi enzi za uhai wake
Gari waliopanda Waandishi hao likiwa chali baada ya kupata ajari
Salaamu za rambi rambi kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro
 


                                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

MWENYEKITI wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’MOROPC’ Nickson Mkilanya ameungana na  Mh Rais   Samia Suluhu Hassan kuomboleza Vifo vya watu 14 wakiwemo Waandishi wa habari 6 wa Mkoani Mwanza.

.

Akitoa rambi rambi hilo leo January 11 Mama Samia alisema watu hao walifari kwenye ajari iliyotoka  leo Mkoani Mwanza.

”Kama mlivyoniona mara kwa mara nilikuwa naongea na simu ni kwamba kuna Waandishi wa habari 6 waliokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyekuwa akielekea Ukelewe  kukagua miradi ya Serikali wamefariki dunia kwenye ajari”alisema Mh Rais na kufafanua zaidi tukio hilo.

 

 Gari lililobeba waandishi hao liligongana na basi dogo na kusababisha vifo vya waandishi  hao na watu wengine waliokuwa kwenye basi hiyo hivyo naomba tusimame kwa dakika moja kuwaombea marehemu hao” alisema Mh Rais.

               
Miongoni mwa waandishi wa habari waliopoteza Maisha ni pamoja na Mtangazaji Mahiri wa ITV na Radio One Mkoani Mwanza  Husna Mlanzi’Pichani enzi za Uhai wake.

 

Pichani ya Pili ni gari  waliokuwa wamepanda Waandishi hao.

 Picha ya tatu ni Salamu za rambi rambi kutoka Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro na Picha ya nne ni Mh Rais Samia Suluhu Hassan.

Makamanda  Mmepoteza Maisha mkilitumikia Taifa leni tangulieni salama tutaonana baadaye.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...