Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
HII haijawahi kutokea, watoto wanaoishi Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo mkoani hapa, jana wamenaswa na kamera za Mtandao huu wakicheza mpira katikati ya Mto mkuu wa Morogoro.
Watoto hao zaidi 20 walifikia uamuzi huo wa kuweka magori na kucheza mpira kwenye mto huo, uliokauka kufuatia mabadiliko tabia ya nchi iliyopelekea Mvua kuchelewa kunyesha msimu huu wa Masika.
Wakizungumza na Mwandishi wa habari hizi Madogo hao walisema.
”Tumeradhimika kucheza hapa Mtoni baada ya Maji kukauka, hali hii inapelekea sisi watoto kukosa maeneo ya kuchezea ili tuibue na kuendelea vipaji vyetu.
Tunaiomba serikali itutengea maeneo ya kucheza hasa wakati huu wa likizo ili kujiepusha na vishawishi vibaya kama vile uvutaji pange na udokozi’wizi’ .
“Kwa upande wao baadhi ya wazee wa Mkoa wa Morogoro walisema historia ya Morogoro Mto huo haujawahi kukauka hata kuwe na ukame kiasi.
“ Yaani hii ni maajabu toka Mkoroni Mto huu haujawahi kukauka hii ndio mara yangu ya kwanza kushuhudia hali hii”alisema Mzee Hamad Chonile ambaye ni Mkulima wa bustani ya Mboga mboga iliyopo shamba la Ustawi wa Jamii akitegemea maji ya mto huo kumwagilia bustani zake.
Mto huo unaotoka Juu ya Milima ya Uluguru unaelekea Mkoa wa Pwani kujiunga na Mto Ruvu kuelekea baharini jijini Dar es salaam.
Hata hivyo jambo hilo ni hatari kwa maisha ya watoto hao kwani ikitoa Mvua kubwa ikinyesha juu ya Milima ya Uluguru Maji Mengi ushuka kwa kasi na kuhatarisha maisha ya watoto hao hasa ukizingatia uwanja wao huo wameujenga kwenye kona kali ya Mto huo.
Clip Video ya watotoa hao wakionyesha vipaji vyao sambamba na kueleza sababau za kucheza Mpira kwenye mto huo itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment