Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 11, 2021

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHO MWA WIKI. MWANAMUZIKI AIMBA HUKU AKIWA JUU YA SPEAK

                Dusheleree akiimba huku akiwa juu ya Speka
                    Dusheleraa Rasta anaye kula mdudu Ngadu
                                        Papaa Kidagala

 Dusheleree na Kidagaa wakiudadafua wimbo wa Mama Mkwe Kisa gani


                Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

Jana mtandao huu uliahidi kurusha habari ya Mwamuziki nyota wa band ya Mikumi Sound ‘Wana Tekenya’ Dushelereee’Rasta anaye kula ngadu’ akiimba wimbo wa Mama Mkwe Kisa gani huku akiwa juu ya Speka.

 

Dusheleree aliimba wimbo huo unaopendwa na wengi akisaidiwa na  Kidagaa[Mwenye kapero kichwani] yeye aliimba akiwa stejini huku kiongozi wake akichana mistari ya wimbo huo akiwa kileleni kwenye moja ya speak za band hiyo.

 Kidagaa na Dusheleree ni wakazi wa Kata ya Chamwino  kata pekee kongwe Manispaa ya Morogoro ambayo haina barabara hata Moja yenye kiwango cha Lami.

Pia kata hiyo ndio inayoongoza kwa kutoa wanamuziki wengi wa Muziki wa Uswazi’Singeli’.

 

Kwa Dusheleree na Kidagaa wao walikacha Singeli na kujikita kwenye Muziki wa dansi ambapo kwa sasa wamejizolea mashabiki wengi Mkoani Morogoro kutokana na umahiri wao wa kutunga na kuimba nyimbo kali kali.

 

Baada ya kunyaka tukio hilo Majira ya saa 7 usiku Mlala Nje alipiga gia Chombo yake na kwenda zake home.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...