Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro'MRFA' Mh Pascal Kihanga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro akizungumza mara baada ya kuzikagua timu.
Kikosi cha Kilombero Soccer Net
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
LIGI daraja la Tatu Mkoa wa Morogoro lmetamatika Jana kwa Mkundi United kuibuka mabingwa, huku Kilombero Soccer Net iliyopewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa huo ikiukosa dakika za za lala salama.
Hatua Hiyo ya mwisho wa ligi hiyo iliyochezwa kwa mtindo ya Point ilijumuisha timu 4 ambazo ni Mkundi, United na Tanzanite Academy kutoka Manispaa ya Morogoro, UDC kutoka Wilaya ya Ulanga na Kilombero Soccer Net toka Wilaya ya kilombero.
Katika kuhakikisha timu hizo hazipangi matokeo kwenye michezo hiyo ya mwisho, Uongozi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ uliamulu michezo hiyo ichezwe Muda mmoja kwenye Viwanja Viwili tofauti, ambapo Tanzanite iliyokuwa na Point 4 ilikipiga na Kilombero iliyokusanya Point 3 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Huku Mkundi iliyokuwa na Point 4 ilikipiga na UDC iliyokuwa na Point 1 huku ikiwa na matumaini ya kupata majibu mazuri kwenye rufaa yao waliokata dhidi ya Tanzanite wakiilalamikia kuchezesha mchezaji asiyesajiriwa kihalali.
Kwa takwimu hizo timu zote 4 zilikuwa na nafasi wa kutwaa ubingwa, katika hatua nyingine Mwandishi wa Mtandao huu aliyekuwa uwanja wa Saba saba majira ya saa 9 na nusu muda mfupi kabla ya michezo hiyo kuanza alimshuhudia Katibu Mkuu wa ‘MRFA’ Emmanuel Kimbawala’Mutu’ akifanya Rotation[Mabadiliko] ya ghafla ya Waamuzi.
Waamuzi wa mchezo wa Jamhuri ambao tayari walishavaa sale wakijianda kuchezesha gemu hiyo waliamuliwa kuingia kwenye gari na sale zao na Katibu huyo na kupelekwa Saba saba kuchezesha mchezo wa Mkundi na UDC na Waamuzi wa Saba saba wakapanda gari la Katibu huyo wakapelekwa Jamhuri Kuchezesha gemu ya Kilombero na Tanzanite.
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye aliweka shushu wake Uwanja wa Jamhuri wakiwasiliana kwa simu mara kwa mara dakika ya 85 alisema Ubao wa Uwanja wa Jamhuiri ulisoma Kilombero 1 Tanzanite 0 muda huo huo dakika ya 85 ubao wa Uwanja wa Saba saba ulikuwa ukiso Mkundi 3 na UDC 3.
Hivyo kama michezo hiyo ingetamatika kwa matokeo hayo Kilombero angekuwa bingwa kwa Point 6.
Kwa mshangao wa wengi Tanzanite walichomoa bao hiyo dakika za mwisho za mchezo na kwamba dakika 90 zilipotimu kwenye viwanja vyote viwili kwa sale, Uwanja wa Saba saba sale ya 3-3 na Uwanja wa Jamhuri Suluhu ya bao 1-1.
Kwa matokeo hayo Mkundi ametwaa ubingwa ikiwa na Point 5 sawa na Tanzanite lakini imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga.
Jana hiyo hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro ‘MRFA’ Mh Pascal Kihanga ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro aliwakabisha Kombe la Ubingwa Mkundi United kwenye Uwanja wa Saba saba.
WAKATI huo huo Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Mchungaji Emmanuel Kimbawala mara baada ya kuwafaurisha waamuzi hao alimueleza Mwandishi wa Mtandao huu. “Shekidele unahabari Uwanja wa Manungu umefungiwa tena baada ya kutokidhi Vigezo kwenye gemu ya Mtibwa na Biashara ambapo gemu hiyo Mtibwa alishinda bao 2-0.
Lakini taarifa njema ni kwamba mara baada ya mvua kunyesha Uwanja wa Jamhuri uko Vizuri hivyo kuna uwezekana mkubwa timu yetu ya Mtibwa ikautumia uwanja huo kwenye gemu ijayo dhidi ya KMC ya Dar”alisema Katibu huyo ambaye pia ni Mwalimu wa shule ya Sekondari Chamwino.
No comments:
Post a Comment