Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, December 9, 2021

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. WANENGUAJI WA BAND YA WALUGURU OG WAPAGAWISHA MASHABIKI.

Wanenguaji wa band ya Waluguru Og wakiwajibika jukwaani
             Rap Muddy akiwajaza Mzuka wanenguaji hao
Kiongozi wa band ya Waluguru Og ambaye pia ni Mmiliki wa band hiyo Deohatius Aruphonce Maarufu Killer Boy Kulia akiimba kwa kushirikiana na Johncena Sukari.' ;Mwana wa Pakaya
                Wanenguaji wakiuwasha Moto Moja Moja




                                        Johncena Sukari


            Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

WANENGUAJI Nyota wa band Pendwa  Mkoani Morogoro ya Waluguru Original, ljumaa iliyopita wameuwasha Moto wa kufa mtu kiasi cha kuwapagawisha mashabiki kibao waliofurika kwenye Ukumbi Mmoja[Jina kapuni] uliopo katikati ya Mji wa Morogoro.

 

Mlala nje akiwa kwenye mishe mishe zake za kusaka matukio kwenye kumbi za Starehe Majira ya saa 4 usiku alitinga kwenye ukumbi huo ulipo jirani na mzunguko wa barabara za Madaraka, SUA,  Kingo na Kenyata na kuwashuhudia wanenguaji wa bendi hiyo waliopendeza kuanzia mavazi hadi Style za Mitindo ya Nywele wakilishambulia jukwaa kwa mitindo mbali mbali  hali iliyokong’a mioyo ya mashabiki lukiki waliojazana kweney Shoo ya bendi hiyo inayoongozwa na Mluguru wa Mkuyuni  Wilaya ya Morogoro Vijijini Deogratius Aruphonce Maarufu ‘Killer Boy’.

 

Mishale ya saa 6 usiku Mlala nje alitoka kwenye kiwanja hicho na kupiga gia Chombo yake ya Mwendo kasi hadi Mazimbu ambapo band ya Mikumi Sound’Wana Tekenya’ wanaotamba na kibao chao Pendwa cha Mama Mkwe Kisa gani walikinukisha ile ile kwenye ukumbi mmoja uliopo pande hizo za Mazimbu.

 

Katika hali ya kushanganza Mlala nje alipotinga kwenye ukumbi huo alimshuhudia Rap Maarufu wa band hiyo Dusheleree akiimba huku akiwa juu ya moja ya Speak za bandi hiyo.

 

Baadae picha za tukio hilo zitaruka hewani hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kwa habari Moto moto za chini ya kapeti.

 
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...