Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, December 16, 2021

UDAKU SPESHO. CHANGUDOA APATA AJARI MBAYA AKIFUNDISHWA BODA BODA HUKU AKIWA AMELEWA.


                       Gari hiyo haihusiani na stori husika


              Na Mdakuzi wa Mtandao wa Shekidele. 

MWANAMKE mmoja Mrembo jina na mahali anapoishi hawavifahamika Mara Moja,anayedaiwa kufanya biashara ‘haramu’ya kuuza Mwili ‘Maarufu Changudoa’ amepata ajari na kuumia vibaya  baada ya kupinduka na boda boda barabara kuu ya Morogoro-Dodoma.

Tukio hilo lililoshuhudia Mubashara na Mdakuzi wa Mtandao huu limetokea Jumapili iliyopita Majira ya saa 12 asubuhi. 

 

Kweli kuna watu wanachezea uhai wao, Mdakuzi alidamka asubuhi na Mapema siku hiyo akiwahi Kanisa la KKKT Usharika wa Kihonda kumpiga Picha Mtoto wa Mfanyabiashara Maarufu aliyekuwa akibatizwa kwenye kanisa hilo ambapo lbada hiyo ya Ubatizo ilipangwa akuanza saa 1 kamili asubuhi.

 

 Mpiga Picha wa Mtandao huu ‘Photo Journalist’anayemiliki kamera za kisasa alipewa tenda na Mfanyabiashara huyo kupiga Picha za Video na za Mgando tukio zima kuanzia nyumbani, Kuelekea kanisani.

 

Hivyo ilibidha Mpiga Picha huyo kudamka 12 asubuhi na kwamba alipofika Kihonda njia Panda ya kuelekea Viwandani, alimuona Mwanaume akimfundisha Mwanamke boda boda huku wote wakionekana kuzidiwa na kilevi Kichwani.

Mashuhuda wa Tukio hilo walimtonya Mdakuzi kwamba wawili hao walikesha kwenye baa moja Maarufu’jina Kapuni kwa sababu za kiuwanaume’ kulipokucha walitoka kwenye baa hiyo na kuingia barabara kuu ya Moro- Dodoma wakifundishana boda boda.

 

“Hii ni hatari sana  Mwandishi wa habari huyu boda boda kakesha disko ukumbi wa[anautaja jina] kanunua huyu Malaya  wote wakiwa wamelewa Jamaa ana mfundisha Pikipiki demu katikati ya barabara”walisema mashuhuda hao.

 

 Wakati Mwandishi akiendelea kuwahoji wananchi hao Mwanamke huyo alipiga gia boda boda hiyo kwa maelekezo ya Jamaa yake na kutimua mbia wakielekea Kihonda.

 Mwandishi naye kapiga gia boda boda yake akaunga tele kwa nyuma kushuhudia Driving School hiyo huku akiwafukuzia kwa lengo la kwenda kuwachoma kwa Trafick wanao kaa njia Panda ya kuelekea Kanisa la Mt Monica Parokia ya Kihonda Maarufu Kanisa la Mangweha.

 

Kabla ya kufika eneo hilo kwenye mteremko  Mkali  jirani na  Shule ya Msingi St Anne Mwanamke huyo alizisha Spidi inayokadiliwa kufika 90 au 100 huku jamaa nyuma akiwa amemkumbatia kiunoni.

 

Walipofika kwenye tuta ‘Bums’ lililopo jirani na Baa ya Vaybe mbele kuna daraja la Ngerengere, kwa vile demu huyo ni lena hakupunguza mwendo kalipanda tuta hilo akiwa na mwendo kasi Pikipiki ikamshinda akaachia Mikono ikaluka juu kama mwewe aliyeopoa kifaranga cha kuku.

 

Jamaa  aliangukia Makalia akasota hatua kama 2 kama mtu anaye wanga huku Mwanamke huyo ambaye hakuvaa kofia ngumu’Helment’ alikuwa na Wigi la elfu 15 kichwani akiangukia kichwa kikadunga kwenye Lami kama Mpira kisha Pikipiki akimwangukia mwilini.

 

 Fasta Jamaa kamnyanyuka huku akisema ‘nyanyuka tuondoke’Mdada huyo Mrefu Mweupe hakujibu chochote, akamnyanyua demu karegea kama mrenda miguu yote miwili ilipinda ikiashiria kwamba imevunjika huku damu zikimtoka Masikioni Puani na Mdomoni na wala alikuwa hali wala haonge chochote.

Kufutia tukio hilo watu walijaa na kuziba barabara hali iliyosababisha magari kushindwa kupita.

 

Mdaku alimshuhudia Jamaa huyo akimbeba demu huyo kama gunia la Viazi Mvilingo na kwenda kumwingiza kwenye daladala ya Kihonda Manyuki, Kondakta na dereva pamoja na abiria wao  wote walishikwa na putwaa huku wakimkodolea Macho  jamaa huyo akimwingia majeruhu huyo kwenye Coaster hiyo.

 

Baadae jamaa huyo kashuka kwenye daladala hiyo fasta kawasha boda boda yake na kukimbia akiwaachia Msale Kondakra na dereva wa gari hiyo.

 

Mdakuzi wa Mtandao huu alipoangalia saa yake ilisoma saa moja kasaro  akapiga gia boda boda yake kuwahi kazi aliyoitiwa  hivyo hakujua mwisho wa siku wenye daladala hiyo mzigo huyo usiokuwa na mwenyewe walikwenda kutua wapi.

               


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...