Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, December 18, 2021

KIPENGELE KIPYA, PAZA SAUTI KERO YA MTAANI KWAKO.

      Lumbesa la takataka likiwa barabarani kwa zaidi ya siku 4

 


                            Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

Mitandao Pendwa ya Shekidele unayosomwa na watu wengi pande zote za dunia www.shekideletz.blogspot.com,lnstagram Facebook kusara 2 ya kwanza shekidele mkude simba ya Pili Dustan shekidele imeanzisha kipengele kipya cha Kero ya Mtaa.

 

 Lengo kuu la kuanzisha kipengele hiki ni kusapoti na kusaidia juhuzi za Uongozi wa halmashauri kuweka Mji wetu  katika hali ya Usafi na Usalama.

 

Naamini  juhuzi zinavyofanywa na Viongozi wetu wa Mkoa za kuuweka mji katika hali ya Usafi na Usalama mbali ya kulinda afya za wakazi wa Mji huo pia juhuzi hizo zina lengo la  kupandisha adhi kutoka halmashauri kuwa Jiji la Morogoro.

Moja ya juhudi zilizofanywa na Uongozi wa halmashauri ya Morogoro ni kufungua Group la la Mtandao wa Whatsap ambalo viongozi wote wa Manispaa.

 Badhia ya Viongozi wa Serikali ya Mkoa Wadau mbali mbali  akiwemo Mwandishi wa habari hizi wameunganishwa kwenye Group hilo laenye lengo la kuibua kero mbali mbali za halmashauri hiyo yenye Kata 29.

 Rais wa awamu ya 5 Marehemu Magufuri alipozinduka Soko  la Morogoro ‘Maarufu soko la Kingalu’ alishangaa kuona mpaka sasa Mkoa wa Morogoro haujawa Jiji huku baadhi ya Mikoa iliyozidiwa Umaarufu na Ukumbwa na Mkoa wa Morogoro ikifudhu Vigezo na kupandishwa Madaraja na kuwa Majiji.

 

Mikoa iliyopandisha kutoka halmashauri na kuwa Majiji kwa miaka ya hivi karibuni ni Pamoja na Jiji la Tanga, Jiji la Dodoma na Jiji la Arusha.  

                      KERO YA KWANZA.

Juzi wananchi wa Mtaa wa Makondeko Kata ya Mwembesoni Manispaa ya Morogoro walipaza sauti kwa Mwandishi wa Mtandao huu wakilalamikia kero ya gari la kuzoa takataka kuchelewa kupita kwenye Mtaa wao.

Hali hiyo ilipelekea wananchi hao kujaza viroba vya takataka kwenye barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabra hiyo inayoelekea kanisa la Kakobe la Mkoani hapa.

 

Wakizungumza na Mtandao kwa Jazba wananchi hao walisema” Zamu yetu ya gari la taka kupita ilikua majuzi lakini chaajabu mpaka leo siku ya 4 gari hilo halijapita na msimu huu ni wa mvua takataka zimeroa zinatoa harufu kali hii.

 

Kwenye pande wa kukusanya pesa hawachelewi hata lisaa limoja”alisema mkazi wa Mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Ally.

 

Alipoulizwa kwa nini wametoa nje takataka hizo na kuzipanga barabarani kabla ya gari halijafika? Mama huyo alijibu

 

“ Chumba change kimoja cha kupanda lundo hili la takataka nitaliweka wapi wakati pesa ya kuzoa takataka tumeshalipa”alisema.

Picha hizo za takataka nimezirusha pia kwenye Group la Whatsap la Manispaa ambapo pia watumishi wengi wa Manispaa hiyo ni wadau wa Mitandao ya Shekidele.

 

Kwa yoyote mwenye kero mtaani wake awasiliane nami kwa namba 0627 48 88 20 au 0782 61 34 45.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...