Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, December 15, 2021

INA UMA SANA. MTOTO WA MCHUNGAJI AFARIKI DUNIA KWENYE AJARI YA PIKIPIKI.

                                Kesheni enzi za Uhai wake

                                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kwa tukio hili nazidi kuamini kwamba tukeshe tukiomba kwa sababu hatujui Siku  wala saa ya kutwaliwa na Mwenyezi Mungu.

 

Jumapili iliyopita  kanisa la KKKT Usharika wa Kihonda Kulikuwa na tukio la Ubatizo, ambapo Mpiga Picha wa Mtandao huu alialikwa kumpiga Picha mtoto wa Mfanyabiashara Maarufu Maeneo hayo ya Kihonda.

 

Mpiga Picha huyo ambaye kanisa lake la kuabudu ni KKKT Usharika wa Mji Mpya, akiwa kwenye lbada hiyo ya Ubatizo, alimuona Class Mant wake wa Darasa la Kipa lmara Usharika wa Mji Mpya Kesheni Mgumba akiimba kwaya Kuu ya Usharika huo wa Kihonda, lfahamike baba yake mzazi Mchungaji Mgumba alikuwa mchungaji Kiongozi wa KKKT Usharika wa Mji Mpya miaka ya nyuma kabla ya kustaafu.

 

Baada ya lbada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo lsaya Kairanga Ole Keiya kukamilika Mwandishi wa Mtandao huu alisamiliana na Kesheni baada ya kutoonana kwa muda mrefu.

 

Kesheni ambaye ni Mzalamo wa Mwanalumango Dar pia ni miongoni mwa watu walioalikwa  kwenye sherehe ya ubatizo wa Mtoto wa Kike wa Mfanyabiashara huyo, Mwandishi wa Mtandao huu na Kesheni walikutana tena  kwenye sherehe hiyo na kupiga stori kwa kirefu.

Miongoni mwa stori hizo Mwandishi huyo alimuliza Kesheni walipo kaka zake Emmanuel Mgumba tulizoea kumwita Bro Emma’ na Ombeni Mgumba, Kesheni akasema Broo Emma yupo hapa hapa Moro na Ombeni ameludi kwao Dar.

 

Sherehe hiyo ilipotamatika tukaagana na Kesheni kwa matumaini kwamba tuyazidi kuwasiliana baada ya kupeana Mawasiliano, chaajabu siku 2 mbele nilipokea taarifa zilizorarua Moyo wangu kwamba Kesheni aliyekuwa akiendesha Pikipiki yake alipata ajari ya kugongana na gari eneo la Mkundi Sheli na kufariki duania.

 

Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe

Kazi ya Mungu haina Makosa, Tulikupenda lakini Mungu wetu amekupenda zaidi.

 

Tangulia rafiki yangu tutaonana baadae,

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...