Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 27, 2021

KUMBUZI YA MIAKA 2 YA KIFO CHA BIBI ALIYEAGA DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 103

                       Bibi Kete Abdallah[103] enzi za Uhai wake
,,,,Bibi Kete akiwa na Mwanaye wa kwanza Tumain Samwel Juma 'Mrs Shekidele'Kulia' kushoto ni Mjukuu wake wa kwanza, William Shekidele ambaye ni Mtoto wa kwanza wa Tumaini.

William anaishi Kigamboni jijini Dar ana watoto 5 na wajukuu 4.

Mwandishi wa Mtandao huu kiulia akipa zawadi ya Rozari Mama yake Mzazi Bi Tumaini Shekidele, ambaye ni Mtoto wa 5 kwenye uzao wa Tumaini aliyejaliwa kuzaa watoto 7. 

Wakwanza William, Wapili Elice'Mrs Riwa' wa tatu Richard, wa nne Rehema'Mrs Magessa. watano Dunstan, 6 Elisante na 7 ni Upendo'Mrs Muchunguzi.

Vicky David Juma 'Mrs Mwambola' akimsaidia bibi yake kukata Keki siku ya Birthday yake ya kutimiza miaka 101 mwaka 2017. sherehe hizi zilifanyika nyumbani kwa bibi Gongolamboto Mombasa Mtaa wa Moshi Baa jijini Dar
...Baada ya kukata keti hiyo akimrisha Mwandishi wa Mtandao huu
Bi Neema Samwel Juma 'Mrs Mulokozi' ambaye ni Mtoto wa tatu wa bibi Kette akimuaga Mpendwa Mama yake aliyefariki dunia Desemba 22 akiwa usingizini akiwa mzima wa afya
Baadhi ya Majirani wakimpa mkono wa Pole Bi Neema ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na Mama yake huyo Mtaa wa Moshi Baa Dar
,,, Baada ya lbada fupi ya kumuombea marehemu iliyofanyika ndani ya hospital ya Amana jijini Dar ambapo marehemu baada ya kufariki dunia mwili wake ulihifadhiwa hapo kwa siku 3 kabla ya kusafirishwa kuelekea Kijijini kwake Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.
....Jeneza lililobeba mwili wa mpendwa bibi yetu likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Lushoto
... Msafara huo ukijianda akuondoka hospital ya Amana
... Msafari huo ukikatiza mitaa ya jiji la Dar kupitia Bagamoyo Road kuelekea Lushoto ambapo Mwandishi wa Mtandao huu aliyeketi siti ya Mbele ya Coaster ya Pili alikuwa bize kupiga Picha matukio yote yakiwemo ya barabarani kutoka Dar Mpka Lushoto
....Msafara huo umetinga daraja la Ruvu Mkoa wa Pwani  barabara kuu ya Chalinze Segera
.... Msafara huo umefika Tarafa ya Mlalo Wilaya ya Lushoro stendi ya Mkongoroni
....David Samwel Juma[aliyeketi ndani ya gari] ambaye ni mtoto wa Pili wa Marehemu Bibi Kette aliyesafiri kutoa Marekani anakoishi  Mpaka Tanga kumzika Mpendwa  Mama yake akizungumza na Mjomba wake William Shekidele kulini ni lkunda Riwa Mtoto wa kwanza wa Elice Shekidele.



Kanisa Kuu la KKKT Usharika wa Mlalom Picha ya hapo juu ni David Juma akiwa nje ya ghorofa la Marehemu baba yake Mzee Samwel Juma mara baada ya Mwili wa Marehemu bibi kette
Mwandishi wa Mtandao huu kushoto kwenye nguo nyekundu, William Shekidele[Kati] na Elisante Shekidele kwa pamoja wakiwa kwenye kaburi la Mpendwa baba yao Mzee Peter Shekidele aliyezikwa kwenye makaburi yaliyopo nje ya Kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo.
...David Juma na Mkewe wakitoa heshima za mwisho kwa Mpendwa mama yao mara baada ya lbada ya kumuombea Marehemu kukamilika kwenye Usharika huo wa Mlalo ambapo enzi za Uhai wake Marehemu Bibi Kette alikuwa Mwimbaji wa Kwaya kuuu ya Usharika huo kabla ya kuhamia jijini Dar kwa watoto zake
Elisante Shekidele na Willia Shekidele wakimbembeleza Mjomba wao David Juma aliyekuwa akimlilia Mpendwa Mama yake
Neema Juma Mrs Mulokozi akitoa heshima za mwili kwa Mpendwa Mama yake Kipenzi, Bi Neema ambaye ni Mstaafu wa hospital ya Hushen Road jijini Dar ndiye aliyekuwa akiishia na Mpendwa Mama yake
,,,,Mwili wa Mpendwa wetu ukitolewa ndani ya kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo Lushoto
...ukielekea nyumbani kwake kwa Maandamano yaliyoongozwa na Kwaya ya Matalumbeta
          Mpendwa bibi kette alizikwa nje ya nyumba yake

David Juma akipanda msibala kwenye kaburi la Mpendwa Mama yake
               David Juma na mkewe wakiweka shada la Maua
Daviid Juma na mkewe wakipiga Picha mara baada ya kuweka shada la Maua kwenye kaburi la Mama yao
                   Neema Mulokozi akiweka shada la Maua
Kitukuu cha kwanza cha Bibi Kette lkunda Riwa akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Mama yake Mkubwa, lkunda ana watoto 2 kama yeye ana mwita bibi Mama Mkubwa sijui watoto zake wanamwitaje bibi Kette wajuzi wa mambo hayo tujuzeni tafadhari
....Baada ya kumpunzisha Mpendwa bibi Kette waombolezaji wakirejea jijini Dar wakiwa katikatika ya Msutu wa Milima ya Usambara wakitokea Lushoto Mjini kuelekea Mombo


 Msafara huo umetua Mombo wakanunua chakula na kuendelea na Safari Picha zote na Dunstana Shekidele.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...