Wamachinga wakipiga shoo bila wasi wasi wowote barabara ya Makongoro iliyopo katikati ya Mji wa Morogoro, Vionavyoonekana Mbele ni Vibanda vipya vya Wamachinga.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WAHENGA wana msemo wao unaosema’Sikio la Kufa halisikia dawa.’ Licha ya Serikali ya ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Wilaya ya Morogoro Mjini ikiongozwa na Mpambanaji kipenzi cha wana Morogoro Mkuu wa Wilaya Mh Albeth Msando.
Kuwaondoa barabarani kistaarabu Wafanyabiashara dogo dogo’Wamachinga’ na kuwahamishia kwenye Vibanda vya kisasa vilivyojengwa nje ya Soko Kuu la Morogoro kwa nguvu binafsi za Mkuu wa Wilaya.
Chaajabu wiki iliyopita Mtandao huu uliwashuhudia baadhi ya wamachinga wamerejea tena barabarani wakipanga bidhaa zao kwenye barabara zilizopo jirani kabisa na Vibanda hivyo.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Mtandao huu walitema nyongo zao wakisema.
”Hawa wamachingana ni Sikio la Kufa licha ya serikali ya Mkoa na wilaya kuwatoa juani walipokuwa wakifanya biashara barabarani na kuwatengenezea Vibanda Vizuri baadhi yao wamegawa biashara zao mara mbili nyingine wamebakiza kwenye vibanda wakiendelea kufanya biashara na nyingine wamekuja kupanga huku barabarani eneo la watembea kwa miguu.
Baadhi ya waswahiri hata uwafanyie ustaarabu kiasi gani hawalidhiki mpaka washurutishwe kibabe hawa wamachingana wamezoea kufukuzwa msobe msobe na Mgambo huku wakitandikwa vilungu na kunyang’anywa bidhaa zao ndio Maisha waliyozoea hawakuzoe maisha haya ya kistaarabu”alisema Hamis Juma.
Miezi kadhaa iliyopita Rais Samia Suluhu Hassan alimtumbua Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Bakari Msulwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bi, Sheila Lukuba, baada ya Mama Samia kuona Clip Video ya Magambo wa Manispaa ya Morogoro wakiwatandika Vilugu Wamachinga waliofanya biashara barabarani eneo la lslam’Maarufu Ghorofa Chafu’ kisha Mgambo hao kumwaga Vyakula vya Mama N’itiliye.
Clip Video hiyo ilipigwa na Mwandishi wa habari Mkoani Morogoro anayepiga Kazi TBC Taifa jina nalihifadhi kwa sababu za kiuwanaume.
Baada ya Viongozi hao kutumbuliwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Martin Shigella alipiga Marufuku Mgambo wote wa Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro kufanya Oparesheni ya kuwaondoa Wamachinga barabarani.
No comments:
Post a Comment