Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, December 24, 2021

HAPPY BIRTHDAY YESU, HAPPY BIRTHDAT SHEKIDELE

Picha ya Mfano Yesu akizaliwa katika Zizi la Ng'ombe Decemba 25 miaka kadhaa iliyopita

            Mwandishi wa Mtandao huu Dunstan Shekidele

HAPPY BIRTHDAY TO ME.

Leo Desemba 25 Wakristo duniani kote wanasheherekea siku kuu ya kuzaliwa Mesiha Yesu Kristo ambaye kwa somo la Mungu kwetu aliluhusu Mtumue huyo aliyekuwa kuukomboa Ulimwengu azaliwe katika zizi la kufungia Ng’ombe kama picha ya mfano inavyoonyesha Mtoto Yesu akizaliwa katika Zizi hilo la Ng’ombe.

Leo Pia Decemba 25 ni kukumbizi ya Kuzaliwa kwa Mwandishi wa Mtandao huu ambaye yeye hakuzaliwa Katika Zizi la Ng’ombe amezaliwa katika Hospital ya Rufaa ya Bombo iliyopo kando kando ya Bahati ya Hindi Jijini Tanga.

 

              SHUKRAN.

Kipekee na Msukulu Mungu kwa kuendelea kunipa zawadi ya Uhai na leo hii kwa Neema zake ameniongezea Mwaka Mwingine.

Pili nawashukuru wazazi wangu Marehemu Baba yangu Mzee Peter Shekidele Mungu amepe punziko   la Aman.

Na Mama yangu Kipenzi Tumaini Shekidele anayeendelea na Matibabu jijini Dar na Muombea kwa Mungu apone upesi.

Tatu nawashukuru Viongozi wote wa dini zote kwa kuendelea kutupa mahubiri na Mawaidha yenye lengo la kutuweka karibu na Mwenyezi Mungu.

 

 Nne nawashukuru Viongozi wote wa Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kuenzi na kudumia Amani inayopelekea mimi na wananchi wengine kuishi kwa amani.  

Tano Nawashukuru ndugu zangu Marafiki zangu na wadau wa Mitandao yangu ya Kijamii hasa Facebook.                        MSAMAHA.

Kupitia siku yangu hii ya kuzaliwa naomba Msahama wa dhati kutoka kwenye sakafu ya Moyo wangu kwa mtu yoyote niliyemkosea kwa kujua au kwa kutoa kujua naomba anisamehe kwani mimi ni kiumbe dhaifu si Malaika.  

 

Pia kupita siku hii nimewasamehe kwa dhati watu wote walionikosema kwa namna yoyote ile.

Happy Birthday Yesu Kristo, Happy Birthday Dunstan Shekidele, Happy Birthday watu wote waliozaliwa siku kama ya leo Desemba 25.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...