Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, December 19, 2021

KERO YA MTAA ILIYORUSHWA JANA NA MTANDAO HUU MBUNGE ABOOD AINGILIA KATI.

        Mbunge Abood alipompigia simu Mwandishi wa Mtandao huu jana Mchana.
 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Baada ya kurusha hewani kero ya Mtaa,Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Aziz Abood ambaye ni msikivu kwenye matatizo ya wananchi wake,alipiga simu kwa Mwandishi wa Mtandao huu akihitaji ufafanuzi zaidi wa Kero hiyo.

 

Mbali na Mh Abood watu mbali mbali  waliupongeza Mtandao huu kwakuanzisha kipengere hichi cha  kero ya Mtaa.

 

Kwa upande wa Vigogo wa Manispaa kupitia Group la Mtandao wa Whatsap baadhi yao waliuliza kero hiyo ipo Mtaa gani ili waweze kuifuatilia kwa haraka. Bila kupepesa Macho kwenye Kero  hiyo  Mwandishi wa habari hizi anatupa lawama kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Wajumbe wake, Ofisa Mtendaji wa Mtaa huo na Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Mara nyingi Viongozi wa Juu akiwemo Rais kwa pamoja wanasisitiza watumishi kutokaa Maofisini wazunguke Mitaani kutatua Kero za wananchi.

 

Kwa Upande wa Mh Abood baada ya Mtandao huu kurusha kero hiyo ndani ya dakika 15 mbele Mbunge huyo kipenzi cha wana Morogoro alimpigia simu Mwandishi wa Mtandao huu akisema.

 

 “Shekidele muda huu nimeingia kwenye Blog yako naona kero ya takataka, hongera kwa kazi nzuri pia nataka kujua taka hizo ziko eneo gani” alisema Mh Abood ambaye pia ni Miongoni mwa Mataji wakubwa Tanzania akimiliki, Mabasi, Malori, Viwanda na Vyombo vya habari ‘Abood Media’   

                             


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...