Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 20, 2021

HATIMAYE LUMBESA LA TAKATAKA LAONDOLEWA BARABARANI

Siku Moja baada ya Mtandao huu kuripoti habari ya lundo la takataka kulundikwa katikati ya barabara Mtaa wa Makondeko Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro na kuibua malalamiko kutoka kwa wananchi

 

Hatiyema taka hizo zimeondolewa na kuifungua barabaraba hiyo inayoelekea kanisa la Kakobe la Mkoani hapa.

 

Leo asubuhi Mwandishi wa Mtandao huu alikatiza kwenye mtaa huo uliopo takribani mita 100 tu na ilipo Ofisi ya  Kata ya Mwembesongo na kushuhudia barabara hiyo ikiwa nyeupe baada ya lumbesa hilo la takataka kuzolewa na Kampuni iliyopewa tenda na Uongozi wa Manispaa kuzoa takataka kwenye Mji huo.

 

Kampuni ya Kampuni ya Kajenyele yenye Makao yake Makuu Jijini Dar es salaam ndio iliyoshinda tenda ya kuzoa takataka kwenye Mji wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...