Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, December 21, 2021

FAINALI LIGI DARAJA 3 MCHEZAJI AMTANDIKA MABUSU MKE UWANJANI.

       Beki huyo akitoka nje ya uwanja baada ya kufunga bao
.....Wachezaji wa hakika wa Kiloe Net wakimkodolea Macho
.                         ......Akikaribia kufika kwa mke wake
                               ...Akimpiga busu mtoto wake
             ...Akimtwanga busu la Mahaba mdomoni mke wake
                        ...Telesia akiwa na Mtoto wake Witness

 Beki Joseph akiwa na familia yake wakati akihojiwa na Mtandao huu Mara baada ya gemu hiyo kukamilika kwa yeye kupiga Hat trick


Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 
 
Hii Kali, 
 
Beki wa kutumainiwa na Mkundi United ya Mkoani hapa, Joseph Barnabasi ‘Maarufu Kulwa’ amewashangaza mashabiki akiwemo Meya wa Mji wa Morogoro Mh Pascal Kihanga, baada ya mchezaji huyo kutoka uwanjani na kumpiga mabusu mkewe Telesia Lucas na Mtoto wake Raitiness.
 
Tukio hilo lililonaswa Live na Mtandao huu limetoka hivi karibuni Uwanja wa Saba saba kwenye fainali za ligi daraja la 3 Mkoa wa Morogoro kati ya Mkundi United na Kilombero Soccer Net. 
 
Katika mchezo huo Mkundi inayofadhiliwa na diwani wa Kata ya Mkundi Mh Seif Chomoka iliibuka na Ushindi wa bao 3 -0 huku mabao yote yakifungwa na Kubwa a.k.a baba Raitness. 
 
Akicheza huku akishuhudiwa na familia yake Kulwa alionyesha kiwango cha hali ya juu ambapo dakika ya 14 alifunga bao la kideo baada ya kupiga Tick taka katikati ya mabeki wa Kilombero na goma kujaa kwenye Net za Kilo Net. 
 
Baada ya kufunga bao hilo Kulwa alikataa kupongezwa na wachezaji wenzake badala yake alitoka nje ya uwanja na kupanda Jukwaani akamtwanga mabusu Mkewe pamoja na mtoto. 
 
Dakika ya 36 Kulwa alifunga bao la Pili kwa kichwa akatoka tena uwanjani na kumtwanga mabusu mkewe pamoja na mwanaye huku wachezaji wa hakiba wa Kilo Net wakikodolea macho tukio hilo.
Hadi dakika 45 za awari zinatamatika Vijana hao wa diwani Chomoka walikuwa mbele kwa bao 2-0.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Kilombero wakihitaji kusawazisha mabao hayo huku Mkundi wakihitaji kuongeza mabao mengine.
Kulwa tena dakika 68 alipanda juu na kukutana na mpira ukizagaa zagaa kwenye eneo la hatari akafumua shuti kali lililojaa wavuni na kuiandikia timu yake bao la 3. 
 
Mchezaji huyo ambaye uwepo wa familia yake uwanjani hapo kulimuongezea Morali ya Upambanaji safari hii hakuweza kupanda jukwaani kumpiga mabusu mkewe baada ya kuwa mbali na Majukwaa kwa kipindi hicho cha Pili tofauti na kipindi cha Pili alikuwa akicheza upande yalipo Majukwaa. 
 
Mara baada ya gemu hiyo kutamatika kwa Mkundi kuibuka na ushindi huo wa bao 3-0, huku Kulwa akipiga Hat trick na kukosa Mpira kama sheria inavyoelekeza. Sheri za soka zinazozimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia’FIFA’ Shirikisho la Mpira Miguu Afrika ‘CAF; na Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania’TFF’ zinaelekeza kwenye ligi za taifa mchezaji akifunga mabao 3 kwenye mchezo 1 apewe zawadi ya mpira. 
 
Kwenye ligi hiyo ya taifa daraja la 3 mkoa wa Morogoro mchezo huyo licha ya kufunga mabao hayo 3’Hat trick’ hakupewa mpira kama sheria inavyoelekeza. 
 
Mara baada ya gemu hiyo kukamilika Mtandao huu ulizungumza na mchezaji huyo pamoja na Mkewe. 
 
Kulwa alisema baada ya kubaini familia yake ipo uwanjani ikimshuhudia akifanya kazi,alicheza kwa juhudi kubwa na alipofanikiwa kufunga mabao hayo aliamu kutoka nje ya uwanjani na kupongezana na familia yake hiyo. Kwa Upande wake Telesia alisema
 
”Leo sikuwa na kazi nyingi nyumbani hivyo nikaamua kuja kushuhudia timu ya Mume wangu akicheza zaidi nimuangalie baba watoto wangu anavyo wajibika uwanjani. Imekuwa kama bahati kwetu kwa mara ya kwanza nakuja uwajanini Mume wangu anaye cheza nafasi za nyuma’Back’ anaisaidia timu kwa kufunga mabao yote 3 nilifurahi baada ya kufunga alikuja huku jukwaani
tukapongezana naye namuombea kwa Mungu Mume wangu afike mbali kisoka”alisema Telesia Lucas aliyejistili vizuri yeye na bint yake.
 
Mahojiano hayo pia ylirekodiwa kwenye Clip Video ambapo pamoja na mambo mengine Mchezaji huyo ameitaja timu ya Simba ya jijini Dar. 
 
Clip hiyo itaruka hewani hivi Punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
 
Wakati Mwandishi wa Mtandao huu akimpiga Picha tukio hilo la Mabusu busu, Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Pascal Kihanga ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro alishindwa kuvumilia akamwita Mwandishi wa Mtandao huu meza kuu na kumuliza
 
”Shekidele tumeshuhudia kila mchezaji wa kundi alipofunga bao alitoka nje ya uwanja ukampiga Picha na yule mwanamke nini kinaendelea kwenye tukio lile kiasi cha kuwa bize kuwapiga Picha.
Hapa Mezani tumekuwa na maswali mengi yasio na majibu tukaamua kukuita Mwanahabari utujuze”alisema Mh Kihanga ambaye pia ni Mfanyabiashara Maarufu wa mbao.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...