Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, November 6, 2021

UKUDAZ SPESHO’ KIMINI CHA MTOA NISHAI MREMBO KATIKATI YA MJI WA MORO.


  Hapa ndio eneo ambalo Mrembo huyo alitumbukia kwenye msingi, baadhi ya watu wakiendelea kumjadi mara baada ya kuondoka


 

                               Na Mdakuz wa Mtandao huu.

 

Dada Mmoja’Mrembo’’Jina linahifadhiwa kwa sababu Maalumu’ Juzi alipata aibu ya kuufunga Mwaka 2021 na kukaribisha Mwaka Mpya wa 2022 baada ya kutolewa nishai na Kinguo kifupi ‘kimini’ alichovaa na kukatiza nacho mitaani.

 

Tukio hilo la aibu ambalo lilishuhudiwa ‘Live bira Chenga na Mdakuzi wa Mtandao huu limetokea jana  katikati ya Mji wa Morogoro barabara ya Madaraka eneo la Lunna kwenye kivuko cha watembea kwa Miguu’Bums.’

 

Mwanamke huyo aliyetinga kigauni hicho kifupi cha Solo ngazi mbili cha tetron   kilichoonyesha sehemu kubwa ya nyeti zake ambapo kila alipokatiza watu walimsema vibaya kwa jinsi alivyokuwa akitembea nusu uchi mchana kweupe tena katikati ya Mji.

 

Alipofika kwenye barabara hiyo akitokea  Upande wa Soko Kuu la Manispaa ya Morogoro Maarufu Soko la Chief Kingalu’wakati akivuka kwenye kivuko hicho cha watembea kwa Miguu,Mama mmoja Mtu mzima alishindwa kujizuia na kuamua kumtupia maneno Mkali Mrembo huyo.

 

”We bint una wazazi na kama una wazazi basi wamekulea kwenye kwapa mbona unatuzaririsha wanawake wenzio kama vipi ungevua kabisa hako kanguo  utembee uchi tujue moja kwamba umechanganyikiwa na Maisha”alisikika Mama huyo akisema huku Mrembo huyo akiendelea kuvuka  Bums hiyo kuelekea upande wa Pili wa barabara.

 

Alipokaribika  kumaliza kuvuka barabara hiyo Mrembo huyo  aligeuka nyuma huku akiwa na hasira akitaka  kumjibu Mama huyo.

 

Chaajabu kabla hajamjibu Mrembo huyo aliyekuwa akitembea huku amegeuka nyuma kumuangalia Mama huyo   alitumbukia kwenye Msingi wa kivuko hicho[Unao onekana Pichani] na  kimini  hicho kilipanda juu ya Kichwa kikanasa kwenye kibani cha nywele zake za rasta hali iliyosababisha nguo yake ya ndani’Chupi’ na Mazagazake yake ya kiunoni yale ya Kimasai kuonekana Mubashara kabla ya wasamailia wema kumuinua na kukichomoa kimini hicho kwenye kibanii na kukishusha na kuishia pale pale juu kabisa ya mapaja yake Manene.

 

Alipoinuliwa Mrembo huyo alilalamika kutenguka Mguu, huku damu zikichilizika kwenye kidole gumba,wakati hayo yanatokea Bi Mkubwa Yule alisogea tena eneo la tukio na kumchana Live Mrembo huyo kwa kumwambia.

 

“ Mungu ni Mkali sauti ya wengi ni sauti ya Mungu kila ulipopita  kila mtu alikunung’unikia na kukushitakia kwa Mungu na Mungu amesikia malalamiko yetu  ndio maana umeanguka kwenye kundi la wanaume  na kubaki uchi”alisema Mama huyo huku Mrembo huyo akiendelea kulalamika maumivu ya Mguu. 

 

Mrembo huyo alipoona watu wanazidi kujazana alijikong’oja akakodi boda boda akatimka zake huku akificha uso.

 

Mdakuzi wa Mtandao huu naye baada ya kukusanya umbeya wote akapiga bederi baiskeri yake akaondoka zake kutafuta Umbeya Mitaa Mingine.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...