Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 4, 2021

SEMU YA PILI NA YA MWISHO MAHOJIANO YA MTANDAO HUU NA BABA MZAZI WA BEKI WA YANGA.

Dickson Job beki tegemo wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania'Taifa Stars'

                                 Nickson Shukuru 'job

 

                                      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Jana tuliishia kwenye swali ambalo Nickson’Shukuru’ Job ambaye ni baba Mzazi wa beki wa Yanga Dickson Job aliulizwa na Mtandao huu.

 

Mwandishi. Unajigawaje sasa kuzitumikia dini hizo mbili za wazazi wako kwa wakati mmoja.

Job. Umeuliza swali zuri, Mimi ni mtoto wa kwanza wa Mzee D -Job baba yangu alipokuwa kwenye mchakato wa kutafuta mke wa kuoa alikutana na Mama yangu Bi Zihaka Salum aliyekuwa akiishi Vibandani Kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro na baba yangu alikuwa akiishi Misufiri.

 

Wakiwa kwenye mchato huo nikazawaliwa mimi baadae baba kasitisha mipango yake ya kumuona Mama kaenda kuona Mkristo mwenzie.

 

Hivyo mimi nikaendelea kulelewa na mama pale Vibandani  akanipa jina la Shukuru ambalo ni la baba yake kwa maana babu yangu Mzaa Mama.

 

Nikiwa shule ya Msingi nikawa naenda  kuswali kwenye Ulemsikiti  wa Vibandani uko jirani na barabara ya Saba saba na kila Mwezi Ramadhan nilijaliwa kufunga.

 

Baadae baba kapata habari hizo akaja kunichukua kanipeleka kanisani nikabatizwa na kupewa jina la Nickson.

 

Kweli majina yote yako hewani siwezi kuyakataa kwa kuwa ni majina niliyopewa na wazazi wangu nikiitwa shukuru naitika vizuri sana ukiniita Nickson pia naitika vizuri sana upande wa Mama wanaita shukuru na upande wa baba wananiita Nickson.

 

Mwandishi. Swali la nyongeza kwenye Maelezo yako hayo mazuri Inaonyesha unazipenda dini zote mbili je kwa sasa unaswali msikitini au unasali kanisani pia sikuombei kifo ila mafundisho ya  dini zote yanasema kila nafsi itaonja umauti je ikitokea umeonja huo umauti utapenda uzikwe na dini gani kati hizo mbili za wazazi wako?

 

Job, Swali gumu sana hilo siwezi kujibu harakaharaka namba nipe muda nitakujibu siku nyingine Shekidele. Mwandishi. Mbona jina lako la Nickson linafanana sana na jina la Mwanao Dickson tofauti ni herufi moja tu ya kwanza

Job.Ni kweli Jina la Dickson ni jina la baba yangu Mkubwa nikaamua kumpa Mwanangu na Mimi nilivyobatizwa baba aliamua kunipa jina hilo la Nickson linalokaribia kufanana na jina la kaka yake.

Mwandishi Ok nashukuru  kwa ushirikiano wako nikiwa jambo lingine nitakupigia simu tuonane tulizungumze.

 

Job Ok karibu sana muda wote wewe ni mtu wangu wa karibu. Kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro jina la Job sio geni kwani Mzee Job alikuwa Maarufu sana akimiliki nyumba za kulala wageni’Gest House’ Maeneo ya Misufini Kata ya Mafiga anamiliki baa Maarufu ya Chipukizi iliyopo Mtaa wa Makongoro Jengo la CCM Wilaya pia yeye ni Mke wake walikuwa waheshimiwa Madiwani kwa miaka Mingi Mzee Job akiwa diwani wa Kata ya Mafiga na Mkewe Mama Job akiwa diwani wa Kata Sultan Area.

 

Takribani Miaka 2 iliyopita Mpendwa wetu Mzee Job ambaye alikuwa shabiki li alia wa Manchester Uinted alifariki dunia mkoani hapa na kuzikwa kijijini kwao Kyela Mkoani Mbeta

                     


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...