Ticha Majuto akihojiwa na Mtandao huu jana huku akiwa ametinga jezi ya timu ya Taifa aliyopewa zawadi na mchezaji wake Kibabage
Beki Kisiki wa Yanga Dickson Job akiwa na Kombe baada ya timu yake ya Moro Kids kutwa ubingwa huo wa Malizni Cup kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KUFUATIA tetezi zinazovuma kwa sasa kama moto wa kifu zinazomhusisha beki wa kushoto wa Yanga Kibwana Shomari, kocha aliyeibua kipaji cha mchezaji huyo Majuto Hamisi’Juto Com’ ametoa neno lililokoleza zaidi moto huyo.
Mara baada ya uvumi huo kuendelea kushika kasi kufuatia Mkataba wa Miaka 2 wa beki huyo na Yanga kuelekea ukingo kuna tetezi zinazodai kwamba Wekundu wa Msimbazi’Simba’ wanamnyemelea mchezji huyo Mzaliwa na Kijiji Cha Kinole Morogoro Vijijini ‘Mluguru Og’.
Kufuatia hali hiyo Jana Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Kocha aliyeibuka Kipaji cha Mchezaji huyo Ticha Majuto kwa lengo la kupata ukweli wa tetezi hizo.
Ticha Majuto alipotakiwa kuelezea tetezi hizo zinazomuhusu mchezaji wake kama zinaukweli wowote au la alijibu kwa ufupi.
”Ni kweli Kibwana mkataba wake na Yanga unakaribia kufika Mwisho, Mpira ni ajira kama ajira nyingine Yanga wakikubali ofa yake atasaidi mkataba mwingine wasipokubaliana atangalia maslaha mazuri timu nyingine”alisema Ticha Majuto na Kuongeza.
” Nimeongea naye baada ya gemu mbili za timu ya taifa kukamilika atakuja hapa Moro akifika nikiwa naye nitakupigia simu Shekidele uje kuzungumza naye kuhusiana na jambo hilo ”alisema kocha huyo wa timu ya kwanza ya Moro Kids ya Under 15.
Kwa sasa Ticha huyo ameibua vibaji vingi hapa nchini kama Vile Kibwana Shomari, Dickson Job [Yanga] na Nickson Kibabage’ anayeitumikia timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni [K.M.C] wote 3 kwa sasa ni wachezaji tegemeo wa timu ya Tifa ya Tanzania Taifa Star’ huku Kibabage akipendelea kuvaa jezi namba 3.
Moja ya jezi hizo za Stars Kibabage alimretea zawadi Ticha wake ambaye wakati akihojiwa na Mtandao huu jana alitinga jezi hiyo huku akithbitisha kwamba amepewa zawadi na Kibabage ambaye ni Mkazi ACACIA Mawenzi Manispaa ya Morogoro.
lfahamike taasisi ya kukuza na kuibua Vipaji vya Moro Youths inatimu 3 timu ya kwanza ni ya watoto wa chini ya miaka 15’Undar 15’ inayofundishwa na Ticha Majuto ya Pili ni ya Vijana chini ya miaka 17 ‘Undar 17’ Maarufu Moro Youths inayofundishwa na Ticha Juma Athuam’Micho’ na ya tatu ni ya Vijana chini ya Miaka 20 ‘Under 20’ Maarufu Moro Kids’ inayonolewa na Ticha Beda.
Kazi Kumbwa inafanywa na ticha Majuto ambaye hutembea Mitaani kusaka watoto wenye vipaji chini ya Miaka 15 na kuwafundisha soka wale wanaofanya vizuri wakifika miaka 17 ana wapandisha timu ya Pili baadae timu ya tatu na mwisho hupelekwa timu za Mtibwa B, Azam B, Ruvu Sooting B na nyingine nyingi.
Kwa habari Moto moto endelea kutembelea Mtandao huu ambapo baadae Picha za Mastaa hao Kibwana na Kibabage zitaruka hewani wakiwa na watoto wachanga
No comments:
Post a Comment