Watu wametumia fursa hiyo kuchimba mchanga mtoni jambo ambalo ni uhalibifu wa mazingira
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WAKATI Wakuu wa nchini mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania wakishiriki Mkutano wa Majadiliano ya Mabadiliko ya Tabia Nchini uliofanyika Nchini Poland, habari ikufikie kwamba baada ya kupita miaka Mingi Mto Mkuu wa Morogoro umenyauka kwa Ukame.
Jana Mwandishi wa Mtandao huu aliyekua akiangalia gemu kati ya timu ya Tanzania’Taifa Star’ dhidi ya Congo DR. kwenye Baa ya Top Ten iliyopo Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa.
Wakati wa Mapunziko Mwandishi huyo aliamua kuzunguka nyuma ya baa hiyo kupunga Upepo kando kando ya Mto huo na kushuhudia Mto huo umenyauka kwa kiasi kikubwa hali iliyopelekea baadhi ya wanchi kuvamia na kuchimba Mchanga kwa lengo la kwenda kufanya shughuli za Ujenzi kama inavyoonekana kwenye moja ya Picha.
Kwa sasa Maeneo Mengi nchini ikiwemo Morogoro Jua ni kali Mno Sambamba na Joto kali nyakati zote asubuhi, Mchana na Usiku.
Kufuatia hali hiyo Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Jiji la Dar’DAWASCO’ hivi karibuni walitangaza Mgao wa Maji kwenye jiji hilo la Maraha ambalo baadhi ya vyanzo vyake vya Maji vinatoka Mkoa wa Morogoro.
Leo Muda huu Mwandishi wa habari hizi ambaye ni mteja wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Morogoro’MORUWASA’amepokea Ujumbe kwenye simu yake kutoka MORUWASA unaosema.
”MORUWASA Inapenda kuwataarifu kutokana na hali ya Ukame kumekuwa na Changamoto za Uzalishaji kwenye Vyanzo vyake vya Maji na hivyo kuathri upatikanaji wa Maji eneo kubwa linalohudumiwa.
MORUWASA inawashauri wateja wake kutumia kwa uangalifu kiasi cha Maji kinachowafikia -tushirikiane kulinda vyanzo vya Maji kwa huduma endelevu”Mwisho wa Kunukuu Ujumbe huo hadi muda huu bado upo kwenye simu yangu.
Kwenye hili hakuna Mwananchi yoyoye atakayekuwa na Malalamiko kwa Mamlaka hizo za Maji nchini kwani kila mtu anaona hali hali ya Ukame kwa vile si watu wote ni wateja wa MORUWASA Mtandao huu umeamua kuweka ujumbe huo wa MORUWASA kwa lengo la kuwasilisha kwa wadau wa Matndao huu ambao sio wateja wa MORUWASA ingawa wanatumia Maji ya Mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment