Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 3, 2021

BABA MZAZI WA BEKI KISIKI WA YANGA AFUNGUKA ALIVYOZITUMIKIA DINI MBILI ZA KIISLAM NA KIKRISTO.

Shukuru Job akihojiwa na Mtandao huu jana huku akiwa ametinga jezi ya Yanga ya Msimu uliopita ambapo mwanaye alimua Kumpa baba yake kama zawadi

                        Beki kisiki wa Yanga Dickson  Nickson Job

                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Nickson Job Maarufu Shukuru ambaye ni baba mzazi wa beki kisiki wa Yanga Dickson Nickson Job amefunguka jinsi alivyozitumikia dini mbili za kiislama na kikristo kwa nyakati tofauti.  

Job amefunguka hayo jana alipofanya Mahojiano Maalumu na Mtandao huu ofisini kwake katikati ya Mji wa Morogoro na mahojiano hayo yalikuwa hivi. 
 
Mwandishi. Kaka Mambo vipi. 
 
Job Powa Shekidele karibu sana ofisini kwangu. Mwandishi. Asante sana hongesa sana naona dogo anafanya kazi nzuri kwenye kikosi cha Yanga. 
 
Job. Namhuskuru Mungu sana kwa hilo. 
 
Mwandishi. Ok tuachane na habari za Mwanao nitakuja siku nyingine unipe histori yake kamili,kama unavyojua mtoto akiwa Star moja kwa moja na mzazi wake naye anaingia kwenye usuper Star.
 
Job.[Kicheko] Ok kwa hiyo unataka nikusaidie nini kwenye habari yako?
 
Mwandishi. Sitaki nizunguke sana swali langu Mama ni kwamba kwa nini unamiliki majina mawili ya dini tofauti yaani Shukuru jina la kiislam na Nickson jina la Kikristo na wote mawili yako hewani kwa maana yote mawili yanatumika? 
 
Job. Mama yangu mzazi Bi Zihaka Salum ni Mluguru wa Pale juu ya Milima ya Uluguru kijijiji cha Keleka dini yake ni Mwislamu na baba yangu Mzazi Mzee Job Patson ni Mnyakyusa wa Kiyela Mbeya ni Mkristo dhehebu la KKKT.
 
Mwandishi. Unajigawaje sasa kuzitumikia dini hizo mbili za wazazi wako? 
 
Job. Mahojiano haya ya kusisimua yataendelea badaye hivyo endelea kuwa jirani na mtandao muda wote usikie majibu ya Job

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...