Na Mwandishi Weyu Morogoro.
LEO nimeamini Utoro kazini, Utoro Shuleni, Utoro nyumba za lbada na Utoro mazoezini sio mzuri.
Nina siku tatu nimetoroka kwenye mazoezi ya timu yangu pendwa wa Moro Veterani.
Leo Jumatatu nimetinga Mazoezi Uwanja wetu wa Moro Sekondari jirani na Chumba cha kuhifadhia Maiti’Mochwari ya Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Nimekuta uwanja Mweupe huku uwanja wa Pili timu ya Moro Kids inayoshiriki ligi daraja la Tatu Mkoa wa Morogoro ikiendelea na Mazoezi.
Nilipouliza nikaambiwa wenzangu wameenda SUA Kucheza mchezo wa kirafiki na moja ya timu zinazojiandaa na Michuano ya SHIMUTA inayotarajiwa kuanza hivi karibuni uwanja wa Jamhuri Mkoani hapa, baada ya ile ya SHIMIWI kukamilika kesho Novemba 2.
Hivyo nikaona nisiludi bure nikaamua kupiga Tizi peke yangu nikazunguka uwanja Round 10 then nikafanya Mazoezi ya viungo ikiwemo Pushap nikiwa na jezi’Uzi’ wa chama langu la Arsenal ambalo juzi lilingina kibabe chumba namba 5 cha ligi kuu England na kumuacha mbali mpinzani wake Mkubwa Manchester United wakiwa chumba namba 8.
Kwa Mujibu wa wataalamu wa Afya duniani kote Mazoezi ni dozi nzuri kwa afya ya binadamu, yanasaidia kuondoa magonjwa mbali mbali yakiwemo yale ya nyemelezi kama vile kisukari, na shinikizo la damu ‘Presha’
USHAURI KWA WADAU WA MTANDAO HUU
Kukaa zaidi ya miezi 3 bila kuutikisa mwili wako ni hatari jwa afya yako
No comments:
Post a Comment