Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, October 17, 2021

MTUMISHI WA MUNGU ANGUSHA MAOMBI MAZITO BARABARANI BAADA YA KUPEWA BETRI.

Mwinjilisi lnnocent Hamda Msafirikulia] akiangusha maombi barabarani baada ya kufanikiwa kupata betri, kushoto ni Mwandishi wa Mtandao huu

 Daada ya kupata betri siku iliyofuata kazi iliendelea kwa kasi ile ile


                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MTUMISHI wa Mungu Mwinjilisti lnnocent Hamad Msafiri juzikati alifanya maombi mazito   eneo la Lunna Mtaa wa Makongoro uliopo katikati ya Mji wa Morogoro akimshukuru Mungu kwa kumuwezesha kupata  Msaada wa betri chakavu la gari litakalomuwezesha kutangaza neno la Mungu Mtaani.

 

Mwinjilisti Hamada ambaye awari alikuwa Mwislamu kabla ya kubadili dini na kuhamia dini ya Kikristo na kupata mujiza ya Utumishi wa Mungu, takribani siku mbili hakufanikiwa kufanya kazi hiyo ya utumishi baada ya betri  la gari analotumia kuwasha vyombo vya muziki kuharibika kwa maana ya kukosa nguvu za kuwasha vyombo hivyo. 

       MUNGU AMFANYIA MIUJIZA.

Wiki iliyopita Mwandishi wa Mtandao huu alikutana na Mtumishi huyo akiwa mnyonge huku akitembea na Miguu tofauti na ilivyozoeleka mara nyingi alitembea na Pikipiki yake akiwa na maspeak nyuma.

Alipoulizwa kwa nini yuko hivyo alijibu

 

”Mtumishi ninasiku mbili sijafanya kazi ya Mungu betri yangu imekufa  kila nikichaji haingizi Moto nimeamua kuacha pikipiki nyumbani, sina uwezo wa kununua betri Mpya nazunguka zunguka hapa mjini kutafuta mtu ninaye mfaahmu mwenye gari nimuombe kama atakuwa na betri mbovu kidogo anipe inisaidi kufanya kazi  ya Mungu  inaniuma sana kutofanya kazi ya Mungu”alisema Mtumishi huyo kwa sauti ya upole.

 

Kauli hiyo ilichoma vikali Moyo wa Mwandishi wa habari hizi, na moja kwa moja akamwambia.

 

” Hapa Mfukoni nina hakiba yangu ya elfu 20 panda baiskeri tuzunguke kwenye magereji  ya marafiki zangu kama watakuwa na betri watuzie kwa kiasi hicho cha pesa.

”Tulianzia gereji ya Sido jamaa zangu wengi walisema hawana betri huku baadhi yao  walikuwa nazo lakini waliuza kwa bei kubwa kuanzia elfu 60 na kuendelea tukashindwa.

 Tukasonge jirani na Sido Simba Oil tukakutana na rafiki yangu mkubwa Samora Mwarabu anayemiliki gereji eneo hilo, tukamueleza shida yetu na kiasi cha pesa tulichonacho”

Mnabahati sana ninasafari ya kwenda Musoma kumsalimia Mama yangu  hivyo juzi tu nimemunua betri mpya na boksi lake hili hapa hii  ikiwa ni maandarizi ya safari hiyo ndefu na betri niliyotoa bado ni nzima sana  kwa vile mtumishi anakweda kufanya kazi ya Mungu nawapa bure shekidele ubarikiwe sana kwa jambo hili hiyo pesa baki nayo tu”alisema Somara na kuongeza.

 

“ Mimi ni fundi kwa kazi anayofanya mchungaji  hii betri pia haitamsaidi sana kwa vile umeme unatoa haujichaji kwa vile hana Otoneka kama zile za kwenye gari umeme unatoka na kujichaji.

 

Chakufanya ili afanya kazi yake vizuri anunua sola  wakati ana hubiri huku betri linajichaji na jua”alishauri Samora.

 

Tuliuchukua ushauri huo tukaingia madukani tukaelezwa kwamba betri Mpya na Sola pamoja na waya zake jumala ni elfu 60.

 

Baada ya mizunguko yote hiyo tukarejea eneo la Lunna na Usafiri wetu wa baiskeri ambapo Mtumishi Hamad alisema.

 

”Mtumishi Mungu akubariki sana  muda huu naomba tufanye maombi ya kumshururu Mungu, sambamba na kuwaombea baraka kwa Mungu wewe na Yule jamaa aliyetupa hii betri’

           OMBI LA MTANDAO HUU. 

Mwandishi wa habari hizi amejitolea hiyo elfu 20 maombi yangu kwa yeyote atakayeguswa na jambo hili achangie chochote ili tufanikishe zoezi hilo la kumnunua Sola Mtumishi huyo ili aweze kutangaza neno la Mungu mitaani kwa uhakika.

 

Atakaye guswa tukio hili  atume chochote atakachojariwa kwa Mtumishi huyo  kupitia namba yake ya Simu 0655 931 534, kwa uhakika kabla ya kutuma unaweza kumpigia  kumueleza dhamira yako.

 

Mungu akijaria tukifanikiwa kununua sola hiyo mtandao huu utaripoti pia tukio hilo kwa lengo la kuwashukuru watakao jaribu kufanikisha zoezi hilo kutoa ni Moyo si utajiri na hakuna mtu aliyefirisika kwa kutoa sadaka kwa Mwenyezi Mungu au kumsaidia mtu mwenye uhitaji.

          

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...