Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 18, 2021

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI, MIKUMI SOUND WAFANYA KWELI.


Star Dushelereee Ras anayekula Ngadu' akiimba wimbo wa Mama Mkwe Kisa gani


 


                Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

BENDI Pendwa ya Mikumi Sound’Wana Tekenya’ ljumaa iliyopita wamefanya makamuzi ya kufa Mtu kwenye ukumbi Mmoja’Jina Kapuni’ uliopo Pande za Mazimbu Mkoani hapa.

 

Chama hilo  Kongwe mkoani Morogoro linaloongoza  kuzarisha wanamuziki wengi nchini kwa sasa linatamba na vibao vyake vikali.

 

‘Mama Mkwe Kisa gani kuninyima mwanao kisa mimi Msambaa. Mama Mkwe Kisa fani Kuninyima Mwanao Kisa Mimi Mchaga’.

Lisong lingine ni  “Wanaosumbuliwa na Mapenzi sio Vibaka tu hata Mapolisi wamo.

Wanaosumbuliwa na Mapenzi sio Wagonjwa tu hata Madaktari wao.

 

 Wanaosumbuliwa na Mapenzi sio Wanafunzi tu hata Walimu wao.

 

 Wanaosumbuliwa na Mapenzi sio Waumini tu hata Viongozi wa dini Wamo.

 

Wanaosumbuliwa na Mapenzi si Mabaa Medi tu hata wamiliki wa baa  wao” hii ni sehemu ya mistari ya nyimbo hizo Pendwa

 

Ngoma hizo mbili ziliwapagawisha vikali mashabiki waliohudhuria show hiyo ya Kibabe iliyonogeshwa na Promotion ya kampuni moja ya Beer nchini.

 

Miongoni mwa waimbaji waliong’ara katika show hiyo ni pamoja na Dusheleree’Rasta anaye kula Ngadu ‘Mwenye Mic Pichani’ambaye sauti yake ya kasuku ilinogesha nyimbo hizo zenye ujumbe makini.

 

lfahamike nyimbo hizo pendwa mkoani Morogoro zimetungwa na Mmiliki wa bendi hiyo Mkongwe Josse Kigenda’Ticha’ ambaye kwa sasa yuko likizi ndefu akijikita kwenye shughuri  binafsi nje ya Manispaa ya Morogoro huku Vijana wake wakiendeleza kazi kwa Viwango vile vile vya T.B.S

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...