Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, October 16, 2021

HUYU SIO RONALD ’CR7’ NI TAJIRI WA TANZANIA AZIZ ABOOD.

Nahodha wa Moro Veterani  Mh Abood akituliza mpira kwenye kifua’Kifriji’ huku akizongwa na Mchezaji wa Reli Veterani Ally Jangalu’kulia’
...Mh Abood akitoka uwanja baada ya kukmalika kazi
Mabasi mapya 20 ya Abood akitua jijini Dar yakitokea China

Weka mbaya na mizengwe ya watu mabasi ya Abood ni noma cheki ndani kama ndege seti ni 2 by 2

                         ...Mzigo umefiia nyumbani Moro


             Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

KATIKA bonanza la uzinduzi wa ofisi ya Kanda la Mashariki lililofanyika Jumapili iliyopita  Uwanja wa Jamhuri Morogoro Kivutia kikubwa alikuwa mchezaji wa timu ya Moro Veterani Mh Aziz Abood ambaye  ni mmoja wa Matajiri wakubwa nchini Tanzania.

 

Abood anamiliki Viwanda, Mabasi, Malori, Vituo vya Mafuta, Maghorofa yenye maduka ya Jumla na Vyombo vya habari’Abood Televishen’ATV’ inayopatikana kwenye king’amuzi cha Star Times na Radio Abood inayosikika vizuri Mikoa ya Morogoro, Tanga, Dar es salaam, Dodoma, Mbeya na Zanzibar.

 

 Mbunge huyo tajiri kipenzi cha Wana Morogoro akiwa na cheo cha Unahodha wa Moro Veterani alitoa mchango mkubwa uwanjani na kufanikisha timu hiyo kabambe ya Moro Veterani kutwaa ubingwa wa bonanza hilo lililoandaliwa na Umoja wa Wachezaji wa zamani Tanzania’UMSOTA’ Taifa.

 

lkumbukwe Mh Abood ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa vipindi vitatu mfurulizo kuanzi uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, 2015 na 2020.

 

Pia Mh Abood ni Kigogo wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro akishikilia nafasi ya’Mnec’ Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa’

 

Katika kuonyesha jeuri wa Pesa Abood juzi Alhams alinunua Mabasi Mapya 20 kwa mpigo ambapo mara baada ya kutua Dar moja kwa moja Mabasi hayo kutoka China yalikuja makao makuu ya Kampuni hiyo Mkoani Morogoro na kwamba yalipofika mzunguko wa barabara wa Msamvu yote 20 yalizunguka mzuko huko kwa Mbwembwe huku yakipiga hoi na kuwasha ‘Double Azad’.

                  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...