Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 11, 2021

MKUU WA MKOA MORO AZINDUA OFISI YA UMSOTA KANDA YA MASHARIKI.

Mgeni rasmi wa akizingua pfisi ya Kanda ya Mashariki ya chama cha wachezaji nyota wa zamanai'UMSOTA'

..Wachezaji nyota wa zamani wakishuhudia tukio hilo kutoka kulia ni Juma Maarufu Anko J. Kati ni Hussein Ngurungu na kushoto ni Sundar Manara


Mgeni rasm Mussa Mnyeti akisalimiana na Mchezaji wa zamani wa Reli ya Morogoro 'Kiboko ya Vigogo' na Simba ya Dar David Mihambo
......Mgeni rasmi akisalimiana na mchezaji wa Moro Veteran Bakari Fungo
Katika bonanza hilo kulikuw ana zoezi la Chanjo ya Covid 19 ambapo baadhi ya wanamichezo hao Wahenga' walijitokeza kuchanja miongoni mwao ni Mzee Hassan Mlapakolo, kwa furaha akionyesha cheti baada ya kuchanja
Mgeni rasm Mussa Mnyeti akizindua Bonanza la wachexaji wa zamani kwa ishala ya kumpa pasi Mchezaji nyota wa zamanai wa Pan na timu ya Taifa Hussein Ngurungu

Mzee Sundar Manara 'Computer' akidrib mpira kuwlwkwa langoni kumsaka Kipa Mzee Mlapakolo.

Kipa namba moja wa zamani wa Sandaland sasa Simba Hassani Mlapakolo akipangua shuti la Sundar Manara

Hata hivyo mshuti huo mkali ulimpalia Mzee Mlapakolo na kuulukia tena akiunyaka kwa style ya kuulalia kama tikiti Maji hali iliyopelekea kidevu chake Cheupe kuoga vumbi la Uwanja wa Jamhuri ambao kwa sasa umefungiwa na TFF kwa kile kilichoelezwa kwamba ni Mmbovu
Mzee Mlapaoko akitamba na Mpira baada ya kunyaka kama nyama shuti la Sundar Manara


Mzee Sundar Manara'Computer' kukokota Mpira dakika i hoi

                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Martine Shigella aliyewakirishwa na Mussa Mnyeti ambaye ni Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Morogoro amezindua Ofisi ya Umoja wa Wachezaji wa Mastaa wa zamani’UMSOTA’ Kanda ya Mashariki.

 

Mara baada ya uzinduzi wa Ofisi hiyo iliyopo nje ya Uwanja wa Jamhuri, kulifanyika Bonanza lililoshirikisha timu 5 za Maveteran kutoka kanda hiyo ya Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na wenyeji Morogoro.

 

Makao Makuu ya ‘UMSOTA’  inayounda Kanda 8 Tanzania Bara yako Mtaa wa lfunda Magomeni jijini Dar kwa mujibu wa  Mwenyekiti wa Taifa wa ‘UMSOTA’ Bw Faza  Lusozi mwishoni mwa mwaka huu wanatarajia kuzindua kanda ya 9 Zanzibar.

 

Timu hizo za Maveterani zilizosheheni wacheaaji nyota wa zamani ni pamoja na Tabata Veterani  kutoka Dar, Moro Veterani, SUA Veterani na Reli Family Veterani zote za Morogoro na ‘UMSOTA’ Taifa.

Katika Bonanza hilo lililofanyika uwanja wa Jamhuri kuanzia Majira ya  saa 3 asubuhi hadi saa 12 jioni timu Kabambe ya Moro Veterani inayoongozwa na nahodha wake tajiri Aziz Abood ilinyakua kombe hilo baada ya kuzitandika bila huruma timu za SUA na Tabata.

 

lfahamike Mwandishi wa habari hizi pia ni mchezaji hatari wa Moro Veterani,nakwamba kwenye bonanza hilo hakushiriki baada ya kupewa jukumu la Kupiga Picha matukio yote ya Bonanza hilo ambalo ndani yake kulikuwa na zoezi la Chonjo ya Covid 19.

 

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye bonanza hilo zikiwemo picha ya Mchezaji wa Moro Vetean mwenye umri wa miaka 71 aliyekusanya kijiji kwenye mmoja wa michezo hiyo na kutoa pasi ya mwisho ya bao ’Asist’.

 

Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kushuhudia matukio hayo zikiwemo picha moja moja za mastaa hao wa zamani kama vile Makumbi Juma,Abas Kuka  Malota Soma,Sundar Juma, Hussein Ngurungu,  Macky Mexime,Sundar Manara’ ambaye pia ni baba mzazi wa Afisa habari wa Yanga Haji Manara na wengine wengi.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...