Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, October 1, 2021

HATARI. WANANCHI WAJAZANA CHINI YA NGUZO ZA UMEME WAKISHUHUDIA MASHINDANO YA MAGARI.


 Magari yakipita spidi kwenye njia za Umeme

             ...Kwenye kona pia kulikuwa na nguzo ya Umeme
Umati wawatu ukiwa chini ya nyaya za Umeme huku wengine wakipanda juu ya Magari yao wakiwa jirani kabisa na Nyaya hizo za Umeme

Mwandishi wa Mtandao huu kulia mwenye kamera nae akiwa eneo hilo lakini kw atahadarri kubwa


 Maafande wa kamtuni ya Ulizmi wakiwa makini kuhakikisha watu hwasogei jirani na eneo hilo la Mbilo za Magari, huku watu hao wakiwa eneo hatarishi zaidi chini ya nyaya za Umeme.


 

                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Katika hali iliyoonekana kuwa ni hatarishi Mashindano ya Magari yamefanyika kwenye nguzo za Umeme huku wananchi wakijazana  chini ya Umeme huo mkubwa wa Greld ya taifa wakishuhudia Mashindano hayo.

 

Mashindano hayo ya Magari yalifanyika hivi karibuni Kata ya Tungi eneo la Nane Nane Tubuyu  Mkoani hapa, kwenye njia za Umeme  unaotoka Kidatu Kilombero Morogoro kuelekea Mikoani mbali mbali nchini.

Siku za nyuma  watu kadhaa walifariki dunia eneo la Mikese baada ya kugongwa na gari wakishuhudia mashindano ya Magari eneo la Kona kali na kwamba moja ya gari  lilipoteza mwelekoa na kuwagonga watu baada ya kushindwa kukata kona.

 

Kufuatia tukio hilo Wandaaji wa Mashindano hayo ya Magari yaliyofanyia  kwenye shamba la Mikonge walijaza maaskali wengi wa kampuni ya Ulizni wakiwazuia watu kusokea jirani  na njia ambazo magari hayo yanapita wakisimama umbali wa takribani mita 50.

 

Hata hivyo Waandaji hao wameshindwa kuchukua tahadhari ya  magari hayo kupita kwenye njia za Umeme sambamba na kuwaondoa watu waliojazana chini ya Nyaya za Umeme huo Mkubwa.

 

lngetokea bahari mbaya moja la gari likapoteza mweleo na kungonga nguzo hizo za Umeme madhara makubwa yangetokea kwa watu waliojazana chini ya umeme huo.

 

Mbaya zaidi wanginge walijiweka kwenye eneo hatarishi zaidi kwa kupanda juu ya magari yao wakizisongelea zaidi vyaya hizo.

 

Ushauri wa Mwandishi wa habari hizi eneo hilo la Shamba la Mikonge ni Kubwa sana wahusika wangeweza kufanya mashindano hayo upande wa kulia au  wa Kushoro ambao uko wazi hauna njia za Umeme kwa Usalama wawatu. Mbaya zaidi moja ya nguzo za Umeme ilikuwa kwenye kona kali hivyo dereva angekosea kidogo mahesabu kwenye kona hilo angeweza kuiangusha nguzi hiyo ya Umeme kwa kuingonga na kusababisha Madhara kwa umati wawatu uliokuuwa chini ya  nyaya za nguzo hizo.

 

MWANDISHI ATIMIZA JUKUMU LAKE.

 

lfahamike kazi kuu ya Mwandishi wa habari ni  Kuhabarisha,Kukosoa, Kuelimisha na Kushauri.

 

Hivyo kwenye tukio hilo Mwandishi wa habari hizi[Mwenye Kamera ambaye naye alikuwa ni sehemu ya watu waliosimama chini ya nyaya hizo za umeme huku akiwa na tahaddari kubwa] amehabarisha na kukosoa pamoja na kushauri.

Tunashukuru Mungu ni Mwema Mashindano hayo yalikwisha salama na hakuna madhara yoyote yaliyotokea.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...