Orezedaa wa band hiyo Killet Boy akiimba Wimbo wa Njia ya Ubena kupitia Chalinze akishirikiana na Rapa wake kushoto, Kati ni Shabiki lia lia wa band hiyo akipagawisha na Wimbo huo wa
Wanenguaji nyota wa bandi hiyo wakiwajibika jukwaani Mmoja Moja
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
BENDI Pendwa ya Waluguru Original ‘Walu Og’ ljumaa iliyopita wamefanya makamuzi ya kufa mtu kwenye ukumbi mmoja’Jina kapuni’ ulipo katikati ya Mji wa Morogoro.
Mlala Nje kama kawa yake Majira ya saa 5 usiku alitinga kwenye ukumbi huo ulipo jirani na mzunguko wa barabara za SUA, Madaraka, Kenyata na Kingo na kushuhudia kikosi kazi cha bendi ya ‘Walu Og’inayomilikiwa na Mluguru wa Mkuyuni Matombo Deogratius Aruphonce Maarufu ‘Killer Boy’ wakifanya yao kwenye kiwanja hicho.
Katika Show hiyo kila idara ilikuwa Bendera Chuma Mlingoti Chuma kwa maana ya wanenguaji walizungusha nyonga kama Feni, Wapiga Vyombo walichana Vyuzi, Ngozi za Dram na Tumba.
Huku Waimbaji wakiongozwa na Prezedaa Killer Boy na Johncena Sukari’Mzee wa Mambo F’lani Sauti zao Matata zilivuma na kupenya Mpaka nje ya Ukumbi na kuangusha Mishikaki Mitamu kwenye Jiko la Papaa Nzige ‘MO’ wa Chama la Black Viba ya Vibandani kwa Mh Diwani Samwel Msuya.
Kivutio kikubwa kwenye Show hiyo ni Wimbo ‘Copy’ wa King Kikii unaonza kwa maneno ya
’Nilikwenda Njia ya Ubena Kupitia Chalinze’ 1 Mkongwe Rhumba Boy ambaye ni Bingwa wa zamani wa kusakata Disko Mkoa wa Morogoro akicharaza Tumba, na kuwapagawisha wanenguaji.
Kufuatia ukali wa bendi hiyo wamepata Mwaliko Jiji la Kitalii la Arusha kuwapagawisha Wachimba Madini wa Mererani.
No comments:
Post a Comment