Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, September 20, 2021

HII KALI YA MWAKA. MTASHA RAIA WA CANADA ADAKWA NA POLISI AKIUZA BUNDUKI 3 KWA ELFU 40.

Kamabda  wa  Polisi Mkoa wa Norogoro SACP Fortunatus Mulisimu akionyesha Silaha hizo.

 

 

                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

MTASHA mmoja raia wa taifa kubwa la Canada Michell Raggy[60]ana shikiliwa na jeshi la Polisi akidai kukutwa na Silaha 3 bukundi aina ya Gobole akizimiliki kinyume cha Sheria na kuziweka sokoni akizipiga bei kwa jumla shilingi elfu 40 na kwa reja reja moja shilingi elfu 50.000.

 

Mcanada huyo ambaye ni Mfanyabiashara hotel kungonwa mkoni Morogoro ya Acropoli iliyopo barabara ya zamani ya Dar es salaam alidakwa Septemba 2 Mwaka huu Majira ya saa 4 asubuhi Mtaa wa Reli Mkoani hapa akiuza magobole hayo kinyume cha Sheria.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

“ Tunamshikiria mtuhumiwa huyo kwa kosa la kukutwa na Silaha 3 aina ya gobole namba  6073A, A5048A, na 5619 A bila kibali, upelelezi ukikamilika tutamfikisha Mahakamani”alisema Kamanda huyo.

 

Kamanda Musilimu pia amethibitisha tukio la Mwanaume mmoja kuvamia ukweli na kuchoma nyumba kwa kile kilichoelezwa kukataliwa na aliyekuwa mpenzi wake.

 

Habari hiyo itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...