Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro akizungumza na Waandishi wa habari jana, mwandishi wa Mtandao huu mwenye nguo nyekuwa naye akiwa bize kukusanya matukio kwenye Press hiyo
.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linawahojiwa wasimamizi 6 wa Mithihani ya darasa la 7 kwa madai ya kutaka kuvujishi Mithihani hiyo kwa wanafunzi waliofanya mithihani hiyo kote nchini Septemba 8 na kumaliza Septemba 9.
Tukio hilo limetokea shule ya Msingi Kamhara iliyopo Wilaya ya Mvomero Mkoani hapa, ambapo wasimamizi hao kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Morogoro wakipangiwa kusimamia kituo hicho.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amewataja wasimamizi hao kuwa ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Juliana Thomas Nyumayo Kabira Mngoni mkazi wa Kamhara.
Msimamizi Mkuu wa Mithihani Anthonia Pastory Mchaga Makazi wa Doma Wilaya ya Mvomero, Msimamizi Mkondo C Francis Kondo Kabila Mkwere Mkazi wa Mkundi Manispaa ya Morogoro na Msimamizi Mkondo A Mwalimu Dorine James Kiwia Mchaga Mkazi wa Madizini Tarafa ya Turiani Mvomero.
Wengine ni Msimamizi Msaidizi B Habibu Hango Mohamed Mwalimu wa Shule ya Msingi Mhonda Mnyiramba Mkazi wa Mhonda Turiani, wa Mwisho ni Mlinzi wa Mithihani kituo hicho cha MG Mohamed Bakuja Koila Mmasai Mlinzi Mfugaji Mkazi wa Kamhara.
”Kuna baadhi ya wanafunzi waliamini uwezo wao ni mdogo hivyo wahusika waliahidiwa pesa kwa lengo la kuwasaidi majibu ambapo watuhumiwa hao walipiga Picha kwa simu zao mithihani hiyo na baadae kuingia kwenye chumba cha Mthihani kuwapa majibu wanafunzi hao.
Kwa vile Jeshi la Polisi tuliimalisha ulinzi mkali tulifanikiwa kuwakamata wahusika kabla ya kuvujisha Mithihani hiyo na tunaendelea kuwa hoji uchunguzi ukikamilika tutawafikisha mahakamani”alisema Big bosi huyo wa Jeshi la Polisi ,Mkoa wa Morogoro. Baadae Mtandao huu utarusha habari ya Raia wa Canada kukamatwa na Silaha 3 hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu mufa wote
‘
No comments:
Post a Comment