Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, September 10, 2021

MKAPKA SASA HAKUNA SHABIKI YOYOTE NCHINI ALIYEFIKIA KIWANGO CHA SHABIKI WA RELI HAYARI LYAMUNGU

                   Shabiki namba moja nchini Hayati Lyamungu

 Uwanja wa mazoezi wa timu ya Reli ya Moro Kibako ya  Vigogo, inayyonekna jirani ni Shele ya Msingi Kaloleni iliyopo mpakani mw akata za Kichangani na Mji Mpya

KUMBUKIZI.

Ukweli usiofichika Tanzania kuna mashabiki wengi wakiwemo wa Simba Yanga na Azam lakini mpaka sasa hakuna shabiki  aliyefikia kiwango  shabiki Maarufu wa timu ya Reli ya Morogoro Hayati Godfrey Hamza Maarufu’Lyamungu’.

 

 Moja ya sifa za hayati Lyamungu  kabla ya gemu alikuwa akijichoma mwili mzima kwa rangi ya mafuta akiandika maneno ya mipasho na kejeri na kubashiri matokeo dhidi ya timu pinzani.

 

Baadhi ya Maneno ya shombo aliyowahi  kujichoro kwenye mwili wake ni siku Reli ilipocheza na Mirambo ya Tabora kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi  alijiandika.”

Mirambo Kumfunga Reli ni Sawa na Jaruo kuimba Taarabu.” Katika mchezo huo Reli aliinyuka Mirambo bao 1-0.

 

Kama hiyo haitoshi Lyamungu ambaye alikuwa pia na mapenzi na timu ya Pan Afrika siku timu hiyo ya Pan ilipocheza na Reli mashabiki wengi mtaani walimuliza atashabikia timu gani kati ya Pan timu yake ya Moyoni na Reli timu yake ya Kazi.

 

Lyamungu aliwajibu watu hao kwa kuingia uwanja akijichora maneno yaliyokuwa na alama ya kuliza

 “Mke na Kazi bora nini? huku akiingia uwanja wa Jamhuri akiwa na bendera ya Reli.

lfahamike toka  Mwandishi wa Mtandao huu anapata akili mpaka sasa haja hajawahi kuipenda timu yoyote zikiwemo Simba, na Yanga zaidi ya Reli ingawa timu hiyo nayo imekufa.

 

Hii ni kwa sababu Mwandishi huyo toka anapata akili akiwa darasa ya kwanza shule ya Msingi Kaloleni iliyopo jirani kabisa na Uwanja wa Mazoezi wa Reli kama  inayoonekana Pichani aliiweka timu hiyo moyoni.

 

Mpaka anamaliza la Saba alikuwa akiangalia mazoezi ya timu hiyo malanyingine kupitia kwenye madirisha ya shule hiyo.

Alipomaliza shule alifanikiwa kupata kadi ya uwachama wa timu hiyo na badae akapati dili la kuwa mpiga Picha wa timu hiyo akizunguka nayo mikoa mbali mbali nchini.

Hayati Lyamungu alifariki Dunia takribani Miaka 10 iliyopita na Pichani   tukiwa  kwenye kambi yetu Dar es salaam hotel ya Shengene  iliyopo Manzese  Tip Top Darajani tukijianda na gemu yetu na Yanga uwanja wa Uhuru Jijini Dar Lyamungu aliniambia

 

”Rafiki yangu Shekidele leo  gemu hii ya Yanga uwanja wa Taifa hapa Dar nakurusha wewe mwili nzima”

 

Tumeingia uwanja wa Taifa Temeke Jijini Dar Reli tuliyepewa jina la Kiboko ya Vigogo kwa kuzifunga Simba na Yanga tutakavyo kwetu Moro mpaka kwao Dar, tulipoingia uwanja wa Taifa’ sasa Uwanja wa Uhuru tulishuhudia umati Mkubwa wa Mashabiki na Moja kwa moja tuliingia uwanjani kila mtu akitimiza majukumu yake Lyamungu akipiga jiramba na wachezaji na Mimi nikiendelea kuwapiga Picha.

Gemu hiyo ilikamilika kwa Reli kuinyuka Yanga bao 1-0 bao hilo pekee likifungwa na Mbuyi Yondani akipokea pasi ya David Mihambo.

Mungu ampunzishe kwa amani anapostahili Mpendwa wetu Lyamungu


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...