Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, August 21, 2021

TWAHA KIDUKU AKATA NGEBE ZA WANA DAR ES SALAAM AMPA SHOW KALI DULLA MBABE NYUMBANI KWAKE.

 

Twaha Kassimu' Twaha Kiduku' Mwana Mji kasoro baharoi aliyepeleka kilio kwa mara ya pili jijini Dar' Show Show'
Twaha Kiduku kushoto kwenye kaptula ya njano akimtwanga makonde Dulla Mbabe bila huruma
'Bendera Chuma Mlingoni Chuma 'Show show' Twaha Kiduku akinyanyulia juju  usiku wa kuamkia  leo baada ya kumtwanga Mpinzani wake mkubwa Dulla Mbabe nyumbani kwake Jijini Dar


                                           Na Dunsta Shekidele,Morogoro.

BONDIA Maarufu nchini mwenye Maskani yake Mtaa wa Mindu eneo la Maskani Manispaa ya Morogoro Twaha Kassim’ Maarufu Twaha Kiduku’ usiku wa kuamkilia leo amekata ngebe za Bondia Dulla Mbabe pamoja na baadhi ya wakazi wa jijini la Dar waliokuwa wakimbeza Kiduku na mkoa mzima wa Morogoro.

 

Katika Pambano hilo la raund 10 lililpigwa ukumbi wa Ubungo Plaza uliopo kando kando ya barabara ya Morogoro jirani na stend ya zamani ya mabasi ya Ubungo Twaha Kiduku ‘Mzee wa Bendera Chuma Mlingoti Chuma Show show’alifanya vibaya raund ya kwanza na raoud 9 zilizofuata  alimpa show kali Dulla Mbabe aliyeonekana zahiri shahili kukata Moto hali iliyopelekea akimbie kimbie hivyo kwenye Ling akikimbia show show ya Kiduku Mjuu wa Bi Lukia Ndege Mtangazaji Maarufu wa Abood Media.

 

Kufuatia hali hiyo ya Kiduku kung’ara kwenye raund 9 na Mbabe aking’ara raund moja tu ile ya kwanza Majaji zote watatu walimpa ushindi Kiduku na kufanikiwa kunyakua zawadi ya ya ‘Ndinga’gari la kisasa Toyota Crawn. 

lnauma sana Mtu kukupiga makonde nyumbani kwako tena mbele ya familia yako na majirani zako, Twaha Kiduku juzi alifunga safari kuelekea Dar na usiku wa kuamkia leo amemtwanga kwa Mara ya Pili Mpinzani wake mkubwa Dulla Mbambe. lkumbukwe Mabonge hao wamepigana mara mbili mara ya kwanza Kiduku alimtwanga Dull Mara ya Pili wakatoka Sale na jana Pambano lao la tatu Kiduku Kamtwanga Dulla. 

Kiduku anauchungu na Dulla kwa vile Dulla Mbambe ndio anayedaiwa kufuta ufalme wa bondia wa Morogoro Francis Cheka abapo Dull alimtwanga Cheka hivyo Twaha anauchungu wa Kaka yake Mwana Morogoro mwenzake kupigwa na Dulla

 

Kama ilivyo ada kabla ya mabondia hao wenye upinzani mkali nchini kama ule wa Simba na Yanga kupanda ulingoni takribani wiki moja nyuma mashabiki wa mabondia hao walitambiani vilivyo huku wale wa Dar wakimbeza Twaha kwamba hawezi kuchukua gari kwa vile Morogoro hakuna barabara barabara ziko Dar.

 

Huku wale wa Morogoro nao wakiwabaza wa Dar wakiwaeleza kwamba Dar hakuna barabara kuna madaraja ya juu ambayo gari hazipiti zinapita ndege wakiwatania kwamba wakizidisha ngebe wananchi hao wa Moro wataamua kuwakatia Maji na Umeme wananchi hao wa Dar ambao kwa asilimia 90 wanategemea Maji na Umeme kutoka Mkoa wa Morogoro.

 

Kwa sasa wananchi wa Mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Viongozi wa juu wa mkoa huo wako kwenye maandalizi mazito ya kumpokea Twaha Kiduku kwa Maandamano  kuanzia Kingolwira Mpaka katikati ya Mji wa Morogoro.

Kabla ya kuondoka kuelekea Jijini Dar juzikati Twaha Kiduku alikutana na kupata Baraka zote za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Martin Shigela, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Albert Msondo, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Mh Hamis Tale tale ‘Babu Tale na baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...