Kiongozi huyo Mkuu wa kabila la Waluguru akizungumz ana Mtandao huu mbele ya Soko Kuu la Morogoro ambalo limepewa jina lake likiitwa Soko Kuu la Chifu Kingali'
Na Dunstan Shekidel,Morogoro.
KIONGOZI wa kimila wa kabila la Waluguru Hussein Ally Mataka Mwenye cheo cha ‘Chief Kingalu wa 15’Mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro na Kijiji cha Kinole Morogoro Vijijini, ameeleza sababau za Soko Kuu la Morogoro kupewa jina lake.
Kihongozi huyo wa kimila amefunguka hayo kwenye mhojiano Maalumu’Exclusive Enterview’ na Mtandao huu.akieleza sababu za Seriakali ya awamu wa 5 iliyoongozwa na Hayati John Pombe Magufuli kutangaza Soko kuu la kisasa la Mkoa wa Morogoro kuitwa jina la Chief Kingalu.
”Mpendwa wetu hayati Magufuli anajua sababu na umuhimu wa kuliita soko hili jina langu”alisema Kwa ufupi kiongozi huyo huku akiwa chini ya Ulinzi Mkali wa Bodgald wake.
Wakati anazindua Soko hilo Mwisho mwa mwaka Jana Hayati Rais Magufuli alisema.
”Soko hili kwa sasa ndio linaloongozwa kwa ubora hapa nchini limetumia zaidi ya Bilion 17 kukamilika kwake.
Nilipofika hapa kunawatu walisema soko liitwe jina la Mkuu wa Mkoa Sanare wengine wakasema liitwe jina la Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mzee Mashishanga namuona yuko hapa kwenye mkutano. Lakini kwa mamlaka niliyonayo namulumu Soko hili kuanzia leo liitwe jina la Chifu wakabila la Waluguru [Soko la Chief
Kingalu]”alisema Hayati Makofuli na kupokea zawadi ya Makofi kutoka kwa wananchi waliofulika kwenye Uzinduzi wa Soko hilo lilipo Kata ya Mji Mkuu katikatika ya Mji wa Morogoro.
Siku zote ukihitaji habari za chini ya Kapeti ambazo huwezi kuzipata Popote tembelea Mtandao huu kila wakati
No comments:
Post a Comment