Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 13, 2021

THE GUNNERS NDONDO CUP, MATAJIRI WA STEND YA MABASI MSAMVU WANG’OLEWA

                              Kikosi cha Chadongo Fc

Kikosi cha Salange kilicho sheheni Mastaa wa Ligi kuu
Zubery Daby kiungo fundi wa  Maafande wa Ruvu Shooting Stars ya Masaubwire
                        Wachezaji wa hakiba wa Salange

                              Heka heka Uwanjani





Mshambuliaji hatari wa Chadogo Fc ambaye ni mchezaji tegeo wa Coastal Union ya jijini Tanga Abdul Seleman Sopu akifunga bao la kwannza check Kamera ya kisasa ya Mtandao huu ulivyonasa bao hilo hatua kwa hatua 
...Kiapa wa Salange Godfrey Mmasa akichupa bila mafanikio 

                            ...Chuma kinagusa nyavu
...Sopu akishangilia bao llake la Pili hata hivyo bao hilo lilikataliwa na Mwamuzi kwa madai kwamba staa huyo wa  Coastal aliotea 
 ...Baada ya kufunga bao hilo la Off Side Sopu alikwenda kuchangia kwenye Bench la Salange ambapo mashabiki wa Salange alimkwida wakitaka kumchapa makonde
                            ....Vulugu hizo zikiendelea huku Mjeshi Zubery Daby[aliyeinua jezi juu mwenye kipara] akishuhudia seke seke hilo

Wakati Vulugu hizo zikiendelea Winga hatari wa Chadogo ambaye pia ni mchezaji tegeo wa Coastal Union ya Jijini Tanga yeye alisogea gorini akapiga stori na Mwandishi wa habari hizi
.... Baadae akamvuta rafiki yake akisema 'Shekidele tutwange Picha'
 Vituko vya Ndondo Cup Mtandao huu ulimshuhudia Kunguru amefungwa nyuma ya gori la Kaskazini mwa uwanja wa Saba saba

 Kipa wa Chadongo Hussein Dior ambaye pia ni Kipa wa Simba B akinyaka Mpira huku  Kiungo wa Salange Zubery Daby naye akinyana mguu wa Kipa huyo, aliyeonyesha kiwango cha juu kwenye michuano hiyo.



                   Dakika ya 90 Salange wamepata Pelnaty 

 Mshambuliaji wa Salange Salum Kihimbwa 'Chuji' ambaye ni Staa wa Mtibwa Sugar akijianda kupiga Mkwaju huyo wa Pelnaty

               ... Akifunga bao na kuisawazishia timu yake 
 

.

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Salange Fc inayomilikiwa na Umoja wa Wasafirishaji wa Stend ya Mabasi Msamvum wamesafirishwa kwenye Michuano ya The Gunners Ndondo Cup’  baada ya kunyukwa na Wauza Vifaa vya Ujenzi Chadongo Fc.  

 

Kati gemu hiyo iliyopigwa Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa, Miamba hiyo yenye nguvu kifedha iliyosheheni wachezaji wengi wa Ligi kuu zilitoka sale ya bao 1-1.

 

 Chadongo wakitangulia kupata bao dakika ya 12 kupitia kwa mshambuliaji wake Abas Abas huku Salange wakichomoa bao hilo dakika ya 90 kwa mkwaju wa Pelnaty iliyofungwa kiufundi wa Salum Kihimbwa ‘Chuji’ Dakika 90 zilipotamatika Mwamuzi wa mchezo huyo Ustadh Shaban Juma aliamulu ipigwe mikwaju ya Pelnaty ambapo Chadogo walifunga Pelnaty zote 5 huku Salange wakikosa moja.

 

Kufuatia Matokeo hayo Chadongo wametinga fainali ambapo leo jioni watakipiga na Wakushi Fc kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa Uwanja  Saba saba

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...