Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, August 1, 2021

GEMU YA HISANI YA KUCHANGIA MATIBABU YA MCHEZAJI WA POLISI YAINGIZA MILIONI MOJA,

                               Mgonjwa Gerald Mathias Mdamu
Mwandishi wa Mtandao huu akiwa na picha kubwa ya Mdamu ambayo ilitumika kuchangisha pesa uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro Jana kwenye mchezo ya hisani kati ya wachezajiza wa VPL na wale wa FDL
 Wadau wa Soka Salum kulia ambaye ni Kiongozi wa timu ya Burkinafaso akiongoza Harambee uwanja wa saba saba jana anyekusanya pesa Kati ni Ustadh Shaban Juma amabye ni Mwamuzi wa ligi daraja la kwanza na anyetoa pesa ni kushoto ni Ticha Mussa Meneja wa timu ya Mawenzi Market
                   Kiongozi wa Salange Fc Edna naye akichangia
...Afisa habari wa Salange Fc naye akizunguka uwanjani hapo akichangisha pesa kwa mashabiki

Wapiga Picha wa luninga ya LTV Hussein Kati na Agrey Kulia nao wakichangia

         Beki wa zamani wa Mawenzi Galas naye akichangia
Wachezaji wa VPL na FDL wakiongozwa na Shuza Jichuya wakipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu wakiwa na Kicha ya Gerald Mdamu


 


                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

GEMU ya hisani ya kuchangia Matibabu ya Mchezaji wa Polisi Tanzania kati ya Wachezaji wanaocheza ligi Kuu’VPL’ dhidi ya wachezaji wanaocheza Ligi daraja la Kwanza’FDL’ imeingia kiasi cha shilingi Milioni Moja.

 

 Gemu hiyo iliyopigwa jana Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa ambayo mgeni rasm alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF Taifa’ Oscar Mirambo.

 

Imeandaliwa na wachezaji nyota wa Ligi kuu na Ligi daraja la kwanza wenyeji wa Mkoa wa Morogoro wakiwa na lengo la kumchangia mchezaji mwenzao Mwana Morogoro Gerald Mathias Mdamu aliyevunjika Miguu yote 2 baada ya basi la Polisi lililopeba wachezaji wa timu hiyo likitokea mazoezi Julai 9 kuelekea kambini lilipata ajari na na wachezaji kadhaa walijeruhiwa huku Madam akiwa ni mchezaji pekee aliyeumia vibaya.

 

Mbali na wachezaji hao wadau mbali mbali wa Mkoa wa Morogoro wakiwemo Waandishi wa habari, Waamuzi wa soka na Viongozi wa vyama vya Soka Mkoa na Wilaya ya Morogoro walishiriki kuanda mchezo huyo wa hisani. 

 

Mara baada ya mchezo huo kukamilika kwa timu hizo kutoka sale ya bao 1-1 Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ni Mmoja wawanakamati wa mchezo huo alizungumza na Katibu Mkuu wa Cha cha Soka Wilaya ya Morogoro Geofrey Mwatesa kwa lengo la kujua kiasi kilichopatikana kwenye mchezo huo ambao mashabiki walilipa kingilio cha buku 2 geni.

”Pale getini tumepata laki 9 na elfu 10, na michango ya uwanjani iliyotolewa na wadau tulipata laki moja na elfu Moja jumla ya pesa yote ni Milion Moja na elfu 11.

 

Tumetoa makato ya matumizi ya mchezo kwa maana ya gharama za Uwanja elfu 40, Maji kwa wachezaji wa timu zote mbili pia tulikodi  Jezi  ghama zote hizo ni shilingi lakini Moja.

 

Hivyo Mgonjwa tutamkabidhi pesa taslimu laki 9, nawashukuru watu wote walifanikisha zoezi hili kipee nakushukuru wewe Shekidele ile picha kubwa ya Mgonjwa tuliitumia kutembeza uwanja kuchangisha pesa kwa mashabiki wengi walipoona Picha ile waliguswa na kuchangia kiasi hicho cha laki Moja”alisema Katibu huyo Mkuu wa MDFA.

 

Baadae Mtandao huu utarusha Picha za Mastaa wote walishiriki  mchezo huo uliochezesha na waamuzi zaidi ya 10 pamoja na Picha ya Mgeni Rasm Kigogo wa TFF Oscar Mirambo alipokagua na kuzungumza na wachezaji wa timu hizo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu Muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...