Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, August 2, 2021

GEMU YA HISANI KUCHANGIA MATIBABU YA MCHEZAJI WA POLISI TZ, MASTAA WA LIGI KUU WABANWA MBAVU NA MASTAA WA LIGI DARAJA LA 1

Kipa wa FDL Salehe Libenanga akifuta bao kwa kunyaka Mpira mkono Mmoja huyu akienda chini. Kipa huyo aliwahi kudakia Mjombe Mji ya Mkoani Njombe inayoshiriki ligi daraja la kwanza
Viongozi Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Oscar Mirambo[Kulia] Mwenye Barako na Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro Geofrey Mwatesa kushoto kwa pamoja wakipiga Picha na Kikosi cha wachezaji wa Ligi Kuuu.
....Viongzoi hao wakiwa na kikosi cha wachezaji wa Ligi daraja la kwanza
...Shiza Kichuya[kushoto mwenye pensi ya Jins akitoa maelekezo kwa wachezaji wa ligi kuu timu iliyocheza dakika 45 za awari
Mgeni Rasm Kigogo wa TFF Taifa Oscar Mirambo akijianda kusalimiana na refa Rashind Ndanje anayechezea ligi kuu  Tanzania Bara
Mkurugenzi wa Ufundi TFF Oscar Mirambo akizungumza na wachezaji wa timu hizo mara baada ya kuwakagua
Kiungo Fundi wa Namungo Mzenji Humud ambaye awari alikuwa Mtibwa Sugar kabla ya kutimkia Namungo ya Lindi
Mohamed Kapeta Mchezaji wa Mbeya City ambaye kabla ya kutimkia Mbeya Mbeya City alikuwa Polisi Morogoro sasa Polisi Tanzania
Beki wa FDL Hamza kushoto akimthibiti Jafar Kibaya wa VPL



...Mshambuliaji hatari wa VPL Jafar Kibaya akijianda kufunga bao
...Akifunga bao hilo huku Kipa wa FDL Saleh Libenanga akidaka upepo
                 ....Kibaya kulia akipongezwa na wenzie

                                    Saleh Libenanga' Libe son'
Reafa Raphael lkambi'Webb' akipuliza kipenga kuashiria kukamilika kwa dakika 45 za awari, refa huyo pia ni wali ligi kuu aliyechezesha nusu fainali ya FA Kati ya Yanga na Biashara gemu hiyo ikipigwa Mkoa Tabora, na juzi alichezesha gemu ya Play Off kati ya Coastal Union na Pamba gemu hiyo ikipigwa jijini Tanga
Baadhi ya mashabiki waliolipa kiingilia cha buku 2 geti kushuhudia gemu hiyo
...Abdallah Wazirti'Kuku' beki wa timu ya JKT Tanzania yenye Maskani yake jijini Dodoma
...Reafa wa 3 kuchezesha gemu hiyo Amin Kihondo akiwajibika uwanjani

..Kipa wa FDL John akipiga shuti huku Shiza Kichuya akimuharas

...Mchezaji huyo wa VPL alikuwa kivutio pia kwenye gemu hiyo
Refa wa 4 kuchezesha gemu hiyo Ally Mnyupe pia wa Ligi kuu ambaye mchezo wake wa mwisho kuchezesha ni kati ya Simba na Coastal Union gemu iliyopita Dimba la Mkapa Temeke jijini Dar

 Mchezaji wa Polisi aliyevunjika Miguu yote miwili Gerald Mathias Mdamu

Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

Mastaa wanaokipiga ligi kuu’VPL’ timu mbali mbali nchini wamebanwa mbavu na Mastaa wanaocheza ligi daraja la kwanza ‘FDL’, kwenye mchezo wa hisani ya kuchangia Matibabu ya Mchezaji wa Polisi Tanzania Gerald Mathias Mdamu aliyevunjika Miguu yote 2 kwenye ajari ya basi la Polisi wakati wachezaji wa timu hiyo wakitoka Mazoezi kurejea kambini Mjini Moshi.

 

Gemu hiyo iliyopiga uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro ambayo pia imehcezeshwa na Waamuzi zaidi ya 10 imekamilika kwa timu hizo kutoka sale ya bao 1-1.

 Kufuatia wingi wawachezaji waliojitokea kwenye mchezo kwa  imeradhimka zigawanywe timu 4 kwa maana wachezaji wa ligi Kuu timu mbili na wale wa daraja la kwanza timu 2 na kila timu itacheza dakika 45.

 

Hivyo timu ya VPL iliyocheza kipindi cha kwanza iliyoongozwa na mchezaji Abdullahaman Humund anayekipiga Namungo, iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya FDL iliyoongozwa na Daud Niyonzima mchezaji wa zamani wa Ndanda ya Mtwara.

 

 Huku bao hilo likifungwa dakika ya 34 na Jafar Kibaya anayekipiga Mtibwa Sugar, Kipindi cha Pili wachezaji wa timu zote mbili walitoka nje, wakaingia wengine na jezi Mpya  ambapo timu ya Pili ya VPL iliongozwa na Shiza Kichuya huku ile ya FDL ikiongozwa na George Chota Mchezaji wa zamani wa Mbeya City.  

 

Hadi dakika 45 za pili zinatamatika Mastaa wa ligi daraja la kwanza wamewwanyuka Mastaa wa Ligi kuu bao 1-0 huku bao hilo likifungwa dakika ya 78 na George Chota, hivyo matokea ya jumla kwa dakika zote ni bao 1-1.

 

Kivutio kwenye mchezo huo ni namna waamuzi nao walivyojitokeza kwa wingi kuchezesha bure mchezo huo kwa lengo lile lile cha kuchangia matibabu ya mchezaji huyom hivyo kutokana na wingi waamuzi hao kila baada ya dakika 22 waamuzi walitoka wakaingia wengine.

 

Wakwanza kuchezesha alikuwa Rashid Ndanje baada ya dakika 22 akatoka na washikavibendera wake, akaingia refa Raphael lkambi’Webb’ akamaliza dakika 23 za kipindi cha kwanza akatoka na wasaidizi wake Kipindi cha Pili akaingia refa Amina Kihondo baada ya dakika 22 akatoka na washikakibendera wake na na dakika 23 za mwishi akachezesha Ally Mnyupe na washikakibendera wake.

 

Kivutio kilikuwa namna waamuzi hao walivyokuwa wakibadilishana huku mchezo ukiendelea bila kuadhiri kitu chochote.

 

Mgeni rasmi kwenye mchezo huo alikuwa Mkurugeniz wa Ufundi wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF Taifa’ Oscar Mirambo.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...