Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, August 8, 2021

BAADA YA KUSOMBA VIKOMBE VYOTE NCHINI WACHEZAJI WA SIMBA KWA SASA WANATIMIZA MAJUKUMU YA FAMILIA, MMOJA AFUNGA NDOA JUZI

                      Injiania Rwanga akiwa na familia yake
MK 14 Meddie Kagera funzia wa kupasia nyavu akiwa na familia yake

 Nahodha Msaidizi wa Simba Tshabalala akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa juzi

. Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Baada ya wachezaji wa Simba ‘Taifa Kubwa’ Mabingwa wa nchini G 4, Wazee wa robo fainali Champion Ligi.

 

 Kukamirisha kwa Mafanikio Makubwa majukumu yao kwa timu yao ya Simba, kwa sasa wachezaji hao wamepewa likizo ya Muda na sasa wamegeukia upande wa pili wakitimiza majukumu ya kifamilia.

 Huku beki Kisiki wa chama hilo  Mohamed Hussein’Tshabalala’ juzi aliihama timu ya Makapera na kujiunga timu bora ya Wana ndoa baada ya kufunga ndoa na Mchumba’ke.

  Pichani Baadhi ya wachezaji wa Wekundu hao wa Mitaa ya Msiambazi Kariakoo jijini Dar, Mnyarwanda Meddie Kagere Raia wa Rwanda,  lnjinia  Rwanga Raia wa Uganda kila mmoja akiwa na familia yake.

 

Na  Mtanzania Tshabalala akiwa na mke wake mara baada ya kufunga pingu za Maisha juzi.

 

Kwa Mujibu wa taarifa kutoka Simba wachezaji wote wa Simba wametakiwa kuripitia leo jumapili na kesho Mazoezi rasmi ya kujianda na msimu Mpya wa ligi yataanza ikiwemo mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga utakaopigwa septemba 25 huku ligi ya Mabingwa Afrika ikipagwa kuanza Septemba 10.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...