Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, August 6, 2021

UDAKUZ WA KITAA WIKI HII.


 


 

 Na Mdukuz wa Mtandao wa Shekidele.

 

Staa wetu wa Morogoro Shiza Ramadhan Kichuya Mkazi wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, uliyepata kuwika na chama kubwa Afrika lenye Maskani yake Mtaa wa Msimbazi nawazungumzaia Simba Taifa Kubwa.

 

Kwa uhodari wako wa kuchonga kona zinazama zenyewe gorini kiasi cha kumtia njaa mtoto wawatu Kipa Ally Mustapha’Barthez’ uliyemfunga Mabao ya Kona akiwa Yanga akatema na kutimkia Singida United ukamfuata huko huko pia ukamfunga bao kama hilo.

 

Kwa Ukari wako Wamanga wa Uarabuni wa.livutiwa na kiwango chako wakaamuka kukununua kwa pesa ndefu ukapiga Soka la Kulibwa Umangani wakiwawakilisha vyema Waluguru wenzako na Wamakonde wenzio.

 

lkumbukwe Kichuya ni Mix Kama kidonge cha kidonge cha rangi 2 Tetasakrin, ukabira  wake ni Pacha baba Mluguru huku Marehemu Mama yake ni Mmakonde ‘Chinga’ kutoka Mtwara.

 

lngawa yeye na machapa wenzie Marehemu Kubwa na Marehemu Doto wamezaliwa na kukulia Mitaa ya Shujaa Kata ya Mji Mpya Morogoro.

 

lfahamike  Hayati Mama Shiza Mungu ampunguzie adhabu ya kaburi kwenye uzao wake huo alijaliwa kuzaa watoto watatu kwa Mpigo wakwanza Kulwa, wapili Doto na wa tatu Shiza huku Kulwa na Doto wakipokuwa elimu ya Msingi walitangulia mbele za haki.

 

lkumbukwe kwa utamaduni wa kitanzania Mama akizaa watoto mapacha wawili au watatu mara nyingi majina yao yanakuwa ya asili  yaani wakwanza anaitwa Kulwa, Wapili Doto na watatu anaitwa Shiza, ikitokea uzao huo wazazi wengi hawapewi nafasi ya kuwapa majina wanayoyapenda watoto wao hao Mapacha..

 

Kwa histori hiyo fupi Staa wetu Shiza Kichuya ambaye kwa sasa unakipiga Cha la Namungo la Ruangwa Lindi kwa  Mh Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwam

 

 Hiyo Simu yako ambayo Mdakuzi wa Mtandao huu  juzikati kwenye gemu ya hisani ya Kuchangia matibabu ya mchezaji wa Polisi Tanzania Uwanja wa Saba saba alikubaba nayo ukiining’iniza kiunoni kwenye Kipenzi chako cha Jins huku ukiwa na flana ya kampuni ya simu ambayo nyuma iliandikwa jina la Kichuya.

 

 Simu hiyo iliibua maswali mengi kutoka kwa mashabiki kibao waliofulika kwenye uwanja huo, wakishindwa kujua kama ni simu ya Upepo ‘Radio Call’ au ni Simu ya kawaida.

 

Wengi walitarajia kwa Ustaa wako ungekuwa na simu Janja ya kupangusa lakini kwa vile hupendahi mbwe mbwe wala huna Makuu licha ya Ustaa wako ambapo unauwezo wa kununua simu yoyote yenye dhamani yoyote lakini unamilika mcheo huo wa sabuni ambao kwa ukubwa wake na urefu wa elya haha mfukoni haika.

 

Kwa leo Mdaku wa Mtandao huu anakomea hapa tukutane wiki ijayo kwa udakuz mwingine.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...