Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, July 18, 2021

HATIMAYE SHISHIMBI ALIYEVUNJWA MKONO NA KIHIMBWA WA MTIBWA SUGAR AFUNGWA BENDEJI NGUMI.

Mchezaji wa Sarange Fc Salum Kihimbwa Chuji' ambaye pia ni mchezaji tegemo ta Mtibwa Sugar akitoa msaada kwa Shabani Shishimbi baada ya kumvunja mkono kwa bahati mbaya waliporuka juu gogombea mpira
                Shambani baada ya kufungwa bendeji ngumu

Sambani Shishimbi siku alivyovunjika mkono kwenye ndondo Cup


 

                        Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

KAMA ambavyo mtandao huu uliripoti awari kwamba utamtembelea mchezaji wa Moro Kids Shabani Shishimbi aliyevunjwa mkono kwa bahati mbaya na mchezaji wa Salange Fc Salum Kihimbwa’Chuji’ ambaye pia ni mchezaji nyota wa Mtibwa Sugar.

 

Jana Mwandishi wa habari hizi alitinga tena nyumbani kwa mchezaji huyo na kuelezwa kwamba toka avunjika mkono hajaonekana nyumbani hapo, Mtandao huu ulimtwangia  simu alivyopokea  aliyesema yuko Mafisa kwenye kambi ya Moro Kids.

Mwandishi wa Mtandao huu alipigia gia Pikipiki yake hadi Mafia na kumkuta beki huyo kisiki wa Moro Kids akiwa na Bendeji ngumu ‘P.O.P.O’ a.k.a Hogo.

 

“Shekidele ubarikiwe sana kwa moyo wako huu toka nipate tatizo umenijari sana huku ukiwa mstari wa mbele kunisaidi kwa kuripoti taarifa zangu kwenye Mitandao yako na Magroup.

 

Kama hiyo haitoshi umefunga safari kuja mpaka huku Mafisa kunijulia hali asante sana kaka” alisema mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa kwenye eneo la ulinzi ambapo kwenye robo fainali hiyo ya michuano ya The Gunners Ndondo Cup Kati ya timu yake ya Moro Kids na Matajiri wa Stend ya Msamvu Salenge Fc  Beki huyo alimthibiti Kihimbwa kwa asilimia 100.

Alipoulizwa kama Kihimbwa aliwahi kumtembelea kwa lengo la kumjulia hali Shabani alijibu kwa ufupi”Toka nivunjike Kihimbwa sijamuona”.

 

 Katika robo fainali hiyo Moro Kids na Salenge Fc walitoka sale ya 0-0 walipotakiwa kupigwa Pelnaty Kipa wa Salange aligoma kwa madai kwamba giza limetanda uwanjani hivyo gemu hiyo ililala kiporo ambapo kwa mujibu wa ratiba timu hizo zitarudiana Alhamis ya Julay 22, huku ile robo fainali nyingine iliyolala kati ya Black Viba na Wakushi Fc yenyewe itapigwa Jumatano ya Julai 21.

 
 

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...