Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, July 22, 2021

MBEYA WA MTANDAO HUU ANASA KERO ZA TOZO ZA MIAMILA YA SIMU MKULIA ACHA MILION 2 KWENYE BASI.

Wakala huyu alikuwa leo akichati baada ya kukaa muda mrefu bila kupta mteja


 

Na Mfukunyuku wa mtandao wa Shekidele.

 

WADAU wote wa mitandao pendwa wa Shekidele, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Ama baada ya salamu ambapo Mtume Mohamad alisema wanaosalimiana wana Kheri mbele za Mwenyezi Mungu.

 

Sasa Mmbeya wa Mtandao huu yuko tayari kukurambia ubuyu aliounasa jana unaohusiana na Tozo Mpya za Mitandao ya Simu za Mkononi nchini Tanzania. Baada ya wabunge kupitiza  sheria ya Tozo  hizo Mpya zinalo zilizoanza kung’ata Julai 15 na kuibua Malalamiko kwa wananchi pande zote za nchini, huku wananchi wengi wakisusia kuweka na kutoa pesa kwenye Miamala hiyo ya simu wakiofika kufyekwa kiasi kikubwa cha pesa tofauti na kile cha awari.

 

Kufuatia hali hiyo  wafanyabiasha na wakulima wamekuwa wakisafiri na lundo la pesa kutoka eneo moja kwenda lingine tofauti na awari walikuwa wakiweka pesa hizo kwenye simu zao kwa vile makato yalikuwa kiduchu. 

        MKULIMA ACHA MILIONI 2 KWENYE BASI.

Jana Mmbeya wa Mtandao akiwa uwanja wa Saba saba alifuatilia michuano ya Ndondo Cup, alimshuhudia Mfanyabiasha wa zao la lriki  akimsimulia mwenzia jinsi alivyosafiri la kiasi kikubwa cha pesa Milion mbili na Mwisho wa siku aliziacha kwenye basi. Baada ya stori hiyo kuwa tamu Mmbeya wa Mtandao huu aliwasogelea jamaa hao na kufungua Masikio yake  yenye ‘Tep Recorda’na kunasa Mbuyu huyo Mwanzo Mwisho.

 

Mfanyabiashara huyo wa lriki alisema kwa muda mrefa anauza lriki hizo Mkoani Njombe na baada ya kupata pesa zake huzitumbukiza kwenye simu na akifika Morogoro anazitoa Maisha mengine yanaendelea.

 

Amesema kufutia tozo mpya za simu ambapo alidai milioni Moja makatoa yake ni zaidi ya shilingi elfu 17 hivyo kwa Milion 2 makato yake ni zaidi ya elfu 30 hivyo kamua kusonda mzigo huo wa Milion 2 kwenye begi lake akapanda basin a begi hilo akaliweka kwenye kelia ya ndani jirani na siti aliyoketi.

 

Ana sema wakiwa basi hilo lilikuuwa likifukuzana na basi linguine kwa lengo la kugombea abiria njiani, anasema  basi lao lilikuwa na mwenzo mkali hivyo lilifanikiwa kuzoa abiria wengi wa njiani.

 

 

Aliendelea kusema miongoni mwa abairia hao kuna mama mmoja alipanda akiwa na mtoto change hivyo kwa vile amejaliwa hekima aliamua kumpisha Mama huyo kwenye siti na kondakta akamuamulua akaketi kwenye tenk la mafuta jirani na dereva.

 

Mfanyabiashara huyo aliendelea kufunguka kwamba walipokaribia Mizani ya Mikumi Kondakta aliwashusha wote waliokosa siti kwenye basi hilo huku akiwaelekeza watembee kwa miguu mpaka mbele ya Mizani.

KWANYE KIPENGELE HIKI MMBEA ANAANZA KUANGUA KICHEKO. 

Upinzania wa  kogombea abiria, Muuza lriki huyo alisema kondakta wa basi lile lingine lililokosa abiria njiani aliamua kuwachoma wenzia kwa maafisa wa Mizani ya Mikumi kwamba wamewashusha abiria njiani waliozidi uzito.

 

Baaba ya kurambishwa ubuyu huo Maafisa hao wa Mizami waliwasa gari lao na kulifuata basi hilo kwa nyuma, katika hali ya kukwepa kukamtwa na kupigwa faini dereva wa basi hilo aliamua kuwapiga abiria wake hao waliopiga mayowe kulisimamisha basi hilo bila mafaniki huku magegi yao yakiwa ndani ya basi likiwemo begi hilo lenye milioni 2. 

Muuza lriki huyo alisema Maafisa hao walilisindikiza basi hilo mpaka mwisho wa Mbuga ya wanyama Mikumi umbari wa takribani kilomita 50.

 

Muuza lriki huyo na wateja wengine walipiga kelele wakilalamikia kuachwa na basi hilo huku mizigo yao ikiwa ndani ya basi.

 

Inadai kufuatia umbari huo Mrefu dereva wa basi hilo aliamua kuwaacha abiria hao na kuendelea na safari huku akiwaamulu wapande mabasi mengine watarejeshewa nauli zao na mabeki yao watayakuta Ofisi za basi hilo Stend ya Msamvu.

 

Mfanyabiashra huyo alisema waligomea ushauri huo huku nao wakidai kwamba wasipowaludia watapiga simu Mizami ya Mikese basi hilo likamatwe.

 

Baada ya mkwala huo dereva alisamimu amri aliamua kuwasubri abiri hao eneo la Doma Mwishi wa Mbuga hiyo ya Wanyama. Muuza lriki huyo alisema yeye na wenzake waliparamia Malori Mpaka Doma.

 

 “Nilipofika Moja kwa moja alikwenda kulichukua begi langi nikalikumbatia Kama nimebeba Mtoto nilipochukulia ndani Milioni 2 zangu zilikuwepo nimeapa sita kubali tena kushushwa kwenye Mizami lakini pia yote hayo ni kutokana na Tozo hizo mpya ya Miamala ya Simu”alisema Mfanyabiashara huyo Mkazi wa Chamwino Morogoro.Jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tubuta, serikali imeunda timu ya wataalamu kupitia upya tozo hizo na kuja na mapendekezo ifikapo Julai 29.

 

Wabunge walipitisha tuzo hizo kwa lengo la seriakli kukusanya kiasi cha shilingi 1-254 tirion katika bajeri ya mwaka 2021-22 serikali ili rekebisha sharia ya Mawasiliano na kielektroniki na Posta CAP306] kwa kuweka tozo kati y ash.10 hadi sh 10,000 katika Miamala ya Simu kulingana na kiasi kitakacho tolewa.

 

Kwa kukokotoa makato hayo inaonyesha kwa kutuma milioni 1 kwa mtu  na kutoa kutagharimu sh 31,000 kama tozo hizo zitahusishwa Watu wengi wanaamini Makato hayo ni Makubwa na wanakwenda kinyume na Mfumo Shirikishi wa kifedha.

 

Hata Rais Samia Suluhu Hassan ameingilia kati jambo hilo na kwamba kwa sasa wasaidizi wake wanatafuta namna sahihi ya kurekebisha jambo hilo linalolamikimiwa na wananchi hapa nchini.


 

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...