Maharusi wakitoka ukumbini huku wakimbungiana Mikono na wageni waalikwa baada ya hafra hiyo kabambe kukamilika
Baadhi ya Madereva wa daladala za Bingwa, Kihonda, Dumila Mkundi, Lukobe, Mazimbu na Mikese wakimbeba juu juu dereva mwenzao wakimpongea kwa kufunga ndoa
Bw Emmanuel Eliniak ambaye ni dereva wa daladala za Dumila- Mjini na Bi Zaina Vuliva ambaye ni Muuguzi ’Nurse’ wa Agape Adiventest Premary School, wamejiondoa kwenye timu dhaifu ya Ukapera a.k.a Usela na kujiunga na timu kabambe ya Wana ndoa inayokubarika duniani na Mbinguni.
Wanandoa hao walipasha Moto Kiporo chao hivi karibuni, jana walifanya hafra kabambe iliyofanyika Ukumbi wa Mango Garden Uliopo Pande za Nungu Manispaa ya Morogoro.
Katika sherehe hiyo iliyoratibiwa kisomi na kuongozwa na lmani ya dini ya Kikristo dhehebu la Sabato, watu walikunywa, Kula na kucheza Muziki Mwanzo Mwisho huku wanakwaya kutoka kanisa la Sabato Misufini wakiongozwa na maharusi pamoja na Mwimbaji binafsi Chiba Son walinogesha sherehe hiyo kwa kutoa burudani kali.
Vile vile nyimbo za asili za kabira la Kipare zilipata nafasi ya kuchezwa kwenye ukumbi huo, lfahamike Bwana harusi na Bibi harusi wote ni Wapare kutoka Mkoa wa Kilimanjaro.
Katika sherehe hiyo Mpiga Picha wa Mtandao huu alibahatika kukutana na Mchungaji Kachua Heliamani anayeongoza kanisa la Sabato Misufini, Mtumishi huyo takribani miaka 10 iliyopita alimfanyia jambo Mpiga Picha wa Mtandao huu jambo hilo ambalo liligeuka kuwa la kuhudhunisha na baadae likageuka kuwa la kufurahisha, kisa hicho nitakurusha hewani hivi punde.
Kama kawaida Mpiga Picha Maarufu wa Mtandao huu ambaye pia ni ‘Photo Journalist’ndiye aliyepewa tenda na Kamati ya Maandalizi kupiga Picha Mtukio yote ya sherehe hiyo ya Kijanja.
Kwa yoyote nayehitaji huduma ya Kupiga Picha bora za Kiwango zaidi ya cha lami kwenye shughuri yake awasiliane na Mpiga Picha wa Mtandao huu anayemiliki Kamera za Kisasa kwa namba 0627 48 80 20 namba ya Watsap 0715 28 90 73.
Bei zake ni nafuu sana pia anatoa ofa kama vile Albam na kurusha hewani kwa ridhaa yako shughuri yako kwenye Mtandao huu unaotazwama na watu wengi pande zote za dunia.
Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu aisimanie ndoa hiyo awaepushe na mabaya yote, wavumiliae madhaifu yao kwa maana ya kubebeana misalama, wakilisimamia kiapo chao cha ndoa cha kupendana mpaka kifo kitakapo watenganisha.
No comments:
Post a Comment