Tepsi ''fundi' wa Mpira akimiliki Mpira mbele ya beki wa Salange juzi kwenye michuano ya The Gunners Ndondo Cup inayoendelea uwanja wa Saba saba Morogoro
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
BAADA ya timu ya lhefu yenye Maskani yake katikati
ya Mashamba ya Mpunga Mbalali Mkoa Mbeya
kushuka daraja kutaka ligi kuu hadi ligi daraja la Kwanza.
Winga hatari wa timu hiyo Tepsi Evance aliyeitumikia
timu hiyo kwa Mkopo akitokea Azam, amesema baada ya timu hiyo kushuka daraja
aikacha timu hiyo na kurejea Azam.
Tepsi Mkazi
wa Kilakala Mkoani hapa aliyasema hayo juzi kwenye uwanja wa Saba saba
aliposhiriki michuano bora ya The Gunners Ndondo Cup, akiitumukia timu ya Moro
Kids iliyokipiga na Salange Fc kwenye mchezo wa Robo fainali.
“Baada ya
lhefu kupanda Ligi kuu Msimu uliopita mabosi wangu wa Azam walinipeleka kwa mkopo hivyo kwa
vile imeshuka daraja nitarejea nyumbani Azam”alisema Winga huyo.
lfahamike kwamba Tepsi akiwa na umri wa miaka 10
alikuwa Academy ya Mwere’ Maarufu Mwere Kids ya Mkoani Morogoro’ inayoongozwa
na Ticha Tike Tike.
Kwenye
michuano ya Vijana chini ya Miaka 17 ya Coca Cola iliyofanyika jijini Dar huku
Tepsi akiitumikia timu ya Mkoa wa Morogoro baada ya michuano hiyo kukamilika,Azam
walivutiwa na kiwango cha mchezaji huyo
wakaamua kumvuta kwenye timu yao kikosi cha Pili na baadae walimtoa kwa Mkopo kwenda lhefu.
No comments:
Post a Comment